-
Iran yazindua makombora ya Emad, Ghadr yaliyoboreshwa
Oct 19, 2025 03:06Kikosi cha Wanaanga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimezindua makombora yaliyoboreshwa ya Emad na Ghadr katika miji ya makombora ya chini ya ardhi.
-
Libya yafanya uchaguzi wa mitaa ulioakhirishwa tangu Agosti
Oct 19, 2025 03:05Tume Kuu ya Uchaguzi ya Libya (HNEC) imetangaza kuanza kwa uchaguzi wa serikali za mitaa katika manispaa 16 nchini kote. Uchaguzi huo ulipaswa kufanyika mwezi Agosti.
-
Mshindi wa Tuzo ya Nobel ampongeza Netanyahu kwa vita dhidi ya Gaza
Oct 19, 2025 03:02María Corina Machado, kiongozi wa upinzani wa Venezuela na Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ametoa shukrani zake za dhati kwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kwa maamuzi yake 'magumu' wakati wa vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza.
-
Mwanasiasa mkongwe wa Kenya Raila Odinga kuzikwa leo
Oct 19, 2025 00:31Mwanasiasa mkongwe na mashuhuri barani Afrika Raila Odinga atazikwa leo nyumbani kwake Bondo.
-
Hizbullah: Vita vya utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya kusini mwa Lebanon vingali vinaendelea
Oct 18, 2025 23:13Mbunge mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon Hizbullah amesisitiza kuwa, vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya maeneo ya kusini mwa Lebanon vingali vinaendelea kwa malengo maalumu na kwa sura tofauti.
-
HAMAS: Hatutajifunga kukabidhi silaha mpaka yatakapofanyika mazungumzo zaidi
Oct 18, 2025 23:12Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesisitiza kuwa haitajifunga moja kwa moja kukabidhi silaha na inatumai usitishaji vita na utawala wa kizayuni wa Israel utadumu kwa muda wa miaka mitatu hadi mitano ili kuijenga upya Ghaza.
-
ICC yatupilia mbali rufaa ya Israel dhidi ya hati za kutiwa nguvuni Netanyahu na Gallant
Oct 18, 2025 23:11Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imekataa ombi la utawala wa kizayuni wa Israel la kukata rufaa dhidi ya hati za kukamatwa waziri mkuu wake Benjamin Netanyahu na aliyekuwa waziri wa vita wa utawala huo ghasibu Yoav Gallant kuhusiana na mauaji ya kimbari yaliyofanywa na jeshi la kizayuni katika Ukanda wa Ghaza.
-
Katibu Mkuu wa UN: Umoja wa Mataifa uko hatarini 'kufilisika' ikiwa nchi wanachama hazitalipa michango yao
Oct 18, 2025 23:11Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuwa umoja huo ulioanzishwa miaka 80 iliyopita unaweza kufilisika ikiwa nchi wanachama hazitolipa michango yao kwa ukamilifu.
-
NAM yaonya kuhusu chokochoko za Washington; Je, Marekani iko mbioni kushambulia Venezuela?
Oct 18, 2025 23:10Wakati ripoti zikionyesha kuwa Pentagon inatayarisha machaguo ya kijeshi dhidi ya Venezuela, Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM), ambayo inaundwa na zaidi ya nchi 120, imeonya kwamba shambulio lolote dhidi ya nchi hiyo ya Amerika Kusini litakuwa ukiukaji wa wazi wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
-
WHO: Hakuna mgonjwa mpya wa Ebola aliyerekodiwa Bulape DRC kwa siku 20
Oct 18, 2025 09:54Ofisi ya Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imetangaza kuwa, hakuna mgonjwa mpya wa Ebola aliyerekodiwa au kuthibitishwa kwa siku 20 katika kanda ya afya ya Bulape, iliyoloko katika mkoa wa Kasai katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako ugonjwa huo umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja.