-
Mabinti barani Afrika watoa wito wa kuheshimiwa haki zao
Oct 13, 2025 02:54Mabinti barani Afrika wametoa mwito wa kuheshimiwa na kupatiwa kipaumbele haki zao za kimsingi. Wito huo umetolewa katika kongamano la kieneo la mabinti magharibi mwa Afrika. Imeelezwa kuwa, haki za mabinti Afrika ni sauti ambayo haiwezi tena kupuuzwa.
-
Iran yakataa mwaliko wa mkutano wa Gaza; yasema haiwezi kuketi meza moja na walioishambulia
Oct 12, 2025 23:40Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekataa mwaliko uliotolewa kwa Tehran kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano kuhusu Gaza uliopangwa kufanyika huko Sharm el Sheikh, Misri akisema kuwa hawezi kuketi pamoja na viongozi waliowashambulia wananchi wa Iran na wanaoendelea kuitishia nchi hii na kuiwekea vikwazo.
-
AU yataka pande hasimu Madagascar kustahamiliana na kufungua mlango wa mazungumzo
Oct 12, 2025 22:58Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) Mahmoud Ali Youssouf jana Jumapili alizitaka pande zinazozozana nchini Madagascar kujizuia na kuvulimiana ili kufungua mlango wa mazungumzo wa kutatuliwa kisiasa mvutano uliozuka nchini humo.
-
Serikali ya Sudan: Waasi wa RSF wameua raia 57 wengine El Fasher
Oct 12, 2025 22:57Serikali ya Sudan imetangaza kwamba shambulizi la droni na ndege zisizo na rubani za Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF limeua raia 57 katika makazi yao ya muda ya mji wa El Fasher wa magharibi mwa Sudan.
-
Ansarullah yaipa muda Israel kuhakikisha inatekeleza kikamilifu usitishaji vita Ghaza
Oct 12, 2025 22:57Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen ameupa utawala wa Kizayuini muda maalumu wa kuhakikisha unaheshimu na kutekeleza makubaliano ya kusimamisha vita vinginevyo Yemen itaanzisha tena operesheni za kijeshi dhidi ya Israel.
-
Waziri wa Vita wa Israel: Tutaharibu mahandaki ya HAMAS baada ya kubadilishana mateka
Oct 12, 2025 22:57Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel ametangaza kuwa utawala huo dhalimu una mipango ya kuharibu mahandaki na njia za chini ya ardhi za Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas huko Ghaza baada ya kuachiliwa huru mateka wa Kizayuni.
-
Je, ni upi msimamo wa Umoja wa Ulaya kuhusu mpango wa Trump na usitishaji vita huko Gaza?
Oct 12, 2025 22:53Umoja wa Ulaya umeeleza kuwa usitishaji vita huko Gaza ni fursa ya kweli ya kuhitimisha vita vya uharibifu.
-
Mkutano wa 8 wa Kimataifa wa Mshikamano na Watoto wa Palestina umefanyika Tehran
Oct 12, 2025 08:59Mkutano wa 8 wa Kimataifa wa Mshikamano na Watoto na mabarobaro wa Kipalestina, umefanyika leo Jumapili kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kiislamu mjini Tehran, kwa kuhudhuriwa na maafisa wa ndani, wageni kutoka nchi za nje na wanaharakati wa Kipalestina.
-
Spika Qalibaf: Serikali na mahakama za kimataifa zifuatilie kesi ya wahusika wa mauaji ya kimbari Gaza
Oct 12, 2025 08:40Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) sambamba na kueleza kuwa usitishaji vita wa Gaza ni kushindwa kwa mipango michafu ya Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni amesema: "Serikali na mahakama za kimataifa zinapaswa kufuatilia kesi ya wahusika wa mauaji ya kimbari huko Gaza."
-
Utawala wa kizayuni wa Israel wafukuzwa katika mashindano ya Dunia ya Jimnastiki
Oct 12, 2025 08:39Ushiriki wa timu ya taifa ya utawala wa kizayuni wa Israel umefutwa katika mashindano ya Dunia ya Jimnastiki ya Jakarta Indonesia kulalamikia jinai za utawala huo ghasibu dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.