-
Olmert akiri: Maangamizi ya kizazi cha Wapalestina yanafanyika Ukingo wa Magharibi
Feb 06, 2026 06:40Waziri Mkuu wa zamani wa utawala wa kizayuni wa Israel Ehud Olmert amekiri kwamba polisi, jeshi na Shirika la Usalama wa Ndani la utawala huo (Shabak) wanahusika katika mashambulizi yaliyopangwa na walowezi dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi, akielezea vitendo hivyo kama njama ya kijinai na utumiaji nguvu ya uangamizaji wa kizazi cha Wapalestina.
-
Tabibu wa viungo: Huenda Trump akawa amebakiwa na miaka 2 hadi 4 tu ya kuishi
Feb 06, 2026 06:40Mtaalamu wa tiba ya viungo Adam James, amezungumzia baadhi ya harakati na alama za kimwili za Donald Trump na kutahadharisha kwamba, huenda rais huyo wa Marekani asiishi zaidi ya miaka miwili hadi minne tu ijayo.
-
Nguesso kuwania tena urais baada ya kuitawala Jamhuri ya Kongo kwa zaidi ya miaka 40
Feb 06, 2026 06:39Rais wa Jamhuri ya Kongo (Brazzaville), Denis Sassou Nguesso, ametangaza kwamba atagombea tena urais wa nchi hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao wa Machi, akiwa na lengo la kusalia madarakani kwa zaidi ya miongo minne huku akiwa na umri wa miaka 82.
-
Araghchi: Iran inaingia kwenye mazungumzo 'ikiwa makini'
Feb 06, 2026 03:17Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amesema Tehran inaingia katika duru mpya ya mazungmzo ya kidiplomasia na Marekani ikiwa hadhiri, makini kabisa na "kwa macho yaliyo wazi."
-
Euro-Med Monitor: EU ni mshiriki wa mauaji ya kimbari Gaza
Feb 06, 2026 02:53Shirika la kutetea haki za binadamu la Euro-Mediteranean Human Rights Monitor (Euro-Med Monitor) lenye makao yake makuu huko Geneva, Uswisi limekosoa vikali msimamo wa Umoja wa Ulaya kwa kuweka masharti yasiyotekelezeka kwa ajili ya ujenzi mpya wa Gaza.
-
AU, UN zalaani mashambulizi ya kigaidi yaliyoua 170 Nigeria
Feb 06, 2026 02:52Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na nchi mbali mbali duniani sambamba na kutoa salamu za rambirambi, zimelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyoua watu wasiopungua 170 magharibi mwa Nigeria.
-
Trump apinga wito wa Putin wa kurefusha muda wa Mkataba wa New START
Feb 06, 2026 02:52Rais wa Marekani, Donald Trump amepinga pendekezo la Rais wa Russia, Vladimir Putin la kuongezwa kwa khiari muda wa Mkataba wa New START, unaoweka mipaka ya silaha za nyuklia, ambao muda wake ulimalizika jana Alkhamisi.
-
HRW: Hali ya haki za binadamu Kenya imeendelea kutia wasiwasi
Feb 06, 2026 02:51Ripoti mpya ya shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) inaonyesha kuwa, hali ya haki za binadamu nchini Kenya ilidorora mwaka uliopita, huku serikali ikikosolewa vikali kwa kukandamiza waandamanaji, wanaharakati, wanahabari na wakosoaji wa serikali.
-
Meja Jenerali Mousavi: Tumeimarisha uwezo wa makombora yetu
Feb 05, 2026 23:26Afisa mwandamizi wa Jeshi wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu imeimarisha mifumo yake ya kujilinda kwa kuboresha makombora ya balestiki yaliyotengenezwa ndani ya nchi.
-
Hamas yalaani mashambulizi ya Israel Ukanda wa Gaza; Netanyahu amekusudia kukwamisha mapatano
Feb 05, 2026 23:00Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imelaani mashambulizi makubwa ya anga ya Israel katika Ukanda wa Gaza yaliyouwa shahidi Wapalestina 23 tangu ustishaji vita wa Oktoba mwaka jana na ksuema kuwa hujuma hiyo ya utawala wa Kizayuni inathibitisha kuwa namna Israel inavyoendeleza kampeni yake ya mauaji ya kimbari.