-
Umoja wa Mataifa kutuma ujumbe wa kusimamia usitishaji mapigano nchini Congo DR
Feb 03, 2026 07:15Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imetangaza kwamba ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Congo utatuma timu yake ya kwanza kusimamia usitishaji mapigano kati ya serikali na muungano wa "Mto Kongo", (Alliance Fleuve Congo) kwa Kifaransa, unaojumuisha harakati ya M-23, katika siku zijazo.
-
Wakenya waendelea kujiunga na vita Ukraine licha ya maafa yanayowapata
Feb 03, 2026 06:48Uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya Wakenya wanaopigana katika vita vinavyoendelea huko Ukraine waliajiriwa kupitia maombi ya moja kwa moja na kampuni moja ya nchini Kenya, ambapo walitakiwa kurekodi video wakieleza nia yao ya kuajiriwa kama wanajeshi.
-
Hamas yatoa wito wa kuchukuliwa hatua za kimataifa za kuvunja mzingiro wa Gaza, kukomeshwa mashambulizi ya Israel, kuhamishwa watu kwa mabavu
Feb 03, 2026 06:27Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ) imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kushiriki katika maandamano ya hasira na shughuli za mashinikizo dhidi ya mashambulizi na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Russia yakosoa vitisho vya Marekani dhidi ya Iran yasema 'havikubaliki'
Feb 03, 2026 05:59Waziri wa Mambo ya Nje wa Ruussiia amesoa vitisho vya Marekani dhidi ya Iran akisema 'havikubaliki' huku Moscow ikitaka kupunguzwa mashinikizo ya Marekani dhiidi ya Iran.
-
Rais Pezeshkian aweka masharti ya mazungumzo na Marekani, 'hakuna vitisho, hakuna mashinikizo'
Feb 03, 2026 04:59Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema amemwagiza waziri wa mambo ya nje kuendelea na mazungumzo na Marekani, alimradi yafanyika katika mazingira ya kuheshimiana na yasiyo na vitisho.
-
Shamkhani: Mazungumzo ya Marekani yanaweza kuzaa matunda iwapo tu yataonyesha heshima, mantiki
Feb 03, 2026 04:40Afisa wa ngazi ya juu wa Iran amesema kuwa mazungumzo yajayo ya nyuklia na Marekani yanaweza kuwa na tija iwapo tu yatajiepusha na anga ya vitisho na madai yasiyo na mantiki, na kusisitiza kuwa Tehran haina nia ya kuhamisha nje ya nchi akiba yake ya urani iliyorutubishwa chini ya makubaliano yoyote.
-
Nigeria yawafungulia mashtaka watu 9 kwa mauaji ya watu 150 mwaka jana huko Yelwata
Feb 03, 2026 04:37Waendesha mashtaka wamewafungulia mashtaka watu tisa kwa makosa ya ugaidi kuhusiana na moja ya mauaji mabaya zaidi yaliyojiri jimbo la Benue mnamo mwezi Juni mwaka jana. Mauaji hayo yalilenga pakubwa jamii ya Yelwata.
-
Taasisi ya Zuma yakadhibisha kuwa na uhusiano na Epstein; yasema ni kampeni chafu dhidi ya Jacob Zuma
Feb 03, 2026 04:31Taasisi ya Jacob Zuma imetoa taarifa kali baada ya jina la rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini kutajwa katika hati mpya za wazi mahakama zenye mfungamana na Jeffrey Epstein, mfadhili na mhusika wa kashfa za ngono aliyefia jela huko Marekani.
-
Ripoti: Israel inashikilia miili 766 ya Wapalestina tangu Oktoba 2023
Feb 03, 2026 04:26Mamlaka za Israel zinashikilia miili ya Wapalestina 766 waliokwishatambuliwa, huku karibu nusu ya miili hiyo ikishikiliwa tangu Oktoba 2023, wakati Israel ilipoanzisha vita vya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza ulio chini ya mzingiro.
-
Ripoti: Iran, Marekani kufanya mazungumzo ya nyuklia mjini Istanbul
Feb 03, 2026 04:23Iran na Marekani zinapanga kufanya duru mpya ya mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran.