Aug 29, 2023 02:46 UTC
  • Makumi ya walowezi wa Kizayuni wavamia msikiti wa al-Aqswa na kuuvunjia heshima

Makumi ya walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya kufurutu ada wamevamia msikiti wa al-Aqswa na kuuvunjia heshima.

Kwa mara nyingine tena walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya kufurutu ada wamevamia msikiti wa al-Aqswa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kulivunjia heshima eneo hilo takatifu lenye historia kongwe.

Walowezi wengi wa Kizayuni wenye misimamo mikali leo wamevamia msikiti wa al-Aqswa kibla cha kwanza cha Waislamu na kufanya vitendo vya kichochezi huku wakiwa wanapatiwa ulinzi na vikosi vya usalama vya utawala haramu wa Israel.

Msikiti wa al-Aqswa unajulikana kuwa nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu na Kipalestina wa eneo takatifu la Quds na utawala wa Israel unajaribu kuharibu utambulisho huo, lakini kusimama imara na kuwa macho wananchi wa Palestina kumeufedhehesha utawala huo wa Kizayuni na kupelekea njama zake kushindwa.

 

Hii si mara ya kwanza kwa walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali kuvamia msikiti wa al-Aqswa wakisaidiwa na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wanaotenda jinai kila uchao dhidi ya ya Wapalestina.

Vitendo vya hujuma za walowezi wa Kizayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqswa vimekithiri zaidi baada ya kuingia madarakani serikali yenye misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu ambayo imekuwa ikionyesha chuki za wazi wazi dhidi ya Wapalestina na maeneo yao matakatifu.

Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Palestina vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyokinzana na utu na ubinadamu.

Tags