Jan 11, 2024 07:46 UTC
  • Al Sudani asisitiza kuondoka haraka wanajeshi vamizi wa Marekani huko Iraq

Waziri Mkuu wa Iraq ameashiria hatua za kuvuruga usalama na amani vya Marekani na kutaka kuondoka nchini humo wanajeshi vamizi wa Marekani haraka iwezekanavyo.

Wananchi, makundi na vyama mbalimbali vya kisiasa huko Iraq kwa miaka kadhaa sasa vinasisitiza juu ya haja ya kuondoka nchini humo wanajeshi vamizi wa Marekani. 

Wanajeshi vamizi wa Marekani wanaendelea kuwepo nchini Iraq katika hali ambayo, viongozi wa Marekani wanakataa kutekeleza majukumu yao kinyume na mazungumzo na makubaliano ya hapo awali kati yao na  serikali ya Iraq. 

Wanajeshi wa Marekani bado wapo Iraq licha ya kufanyika duru kadhaa za mazungumzo ya kistratejia kati ya Baghdad na Washington kwa ajili ya kuhitimisha uwepo wa wanajeshi wa Marekani huko Iraq kufuatia kumalizika vita dhidi ya kundi la Daesh na kupasishwa mpango wa kuwaondoa wanajeshi wote wa Marekani huko Iraq. 

Wanajeshi vamizi wa Marekani huko Iraq 

Kuhusiana na hili, Mohammed Shia al Sudani Waziri Mkuu wa Iraq amesema kuhusu uwepo wa vikosi vamizi vya Marekani nchini humo kwamba: Baghdad inafanya jitihada ili kuhitimisha haraka na kwa utaratibu uwepo wa wanajeshi wa muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani  huko Iraq ili wanajeshi hao wasibaki nchini humo kwa muda mrefu na wasikabiliwe na mashambulizi. 

Tags