Mar 21, 2024 02:11 UTC
  • Israel: Tumeua watu 90 katika Hospitali ya al-Shifa

Jeshi la utawala haramu wa Israel limekiri na kutangaza wazi kuwa askari wake wameua Wapalestina 90 katika uvamizi na hujuma ya siku mbili katika Hospitali ya al-Shifa huko katika Ukanda wa Gaza.

Aidha taarifa iliyotolewa jana Jumatano na jeshi hilo la Kizayuni imeeleza kuwa, wanajeshi wa utawala huo pandikizi wamewateka nyara watu 160 waliokuweko kwenye hospitali hiyo.

Utawala wa Kizayuni umejikanganya kwa kudai katika taarifa hiyo kuwa, wanajeshi wake wamezuia maafa ya kibidamu hospitalini hapo, na kwamba wametwaa silaha zilizokuwa hapo mbali na 'kuwasaili' watu 300.

Kwa siku mbili mfululizo, vikosi vya jeshi la utawala wa Israel vilivyojizatiti kwa silaha nzito vimevamia Hospitali ya al-Shifa katika mji wa Gaza kwa kutumia vifaru na ndege zisizo na rubani na kuwafyatulia risasi watu waliokuwa ndani ya jengo hilo.

Wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni kuanzia Jumatatu asubuhi waliishambulia Hospitali ya al-Shifa katika Ukanda wa Gaza; na mbali na kuwauwa shahidi makumi ya raia wa Kipalestina, wamepelekea mamia ya wengine kuwa wakimbizi, huku wakiwazingira wagonjwa, waandishi wa habari, madaktari na wahudumu wa afya ndani ya hospitali hiyo.  

Ukatili wa Israel dhidi ya Hospitali ya Shifa

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, watu wapatao 30,000, wakiwemo raia waliopoteza makazi yao, wagonjwa waliojeruhiwa na wahudumu wa afya wamekwama ndani ya hospitali hiyo ya al-Shifa.

Uhalifu huo mpya wa kivita umeongeza rekodi nyingine chafu katika faili jeusi la jeshi vamizi linalokalia ardhi za Wapalestina kwa mabavu, na ambalo lingali linafanya uhalifu na mauaji mengi, na linaendelea kuiangamiza sekta ya afya na kuharibu hospitali katika Ukanda wa Gaza uliowekewa mzingiro.

Tags