May 10, 2024 10:10 UTC
  • Abdul Malik al-Houthi
    Abdul Malik al-Houthi

Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen, Abdul Malik al-Houthi, amesema vikosi vya jeshi la nchi hiyo vitalenga meli za kampuni yoyote inayohusiana na kusambaza au kusafirisha bidhaa hadi Israel bila kujali zinakoelekea.

Hii inatambuliwa kuwa ni hatua ya nne ya kulipiza kisasi "uchokozi wa Israel dhidi ya Rafah" kusini mwa Ukanda wa Gaza, lakini Yemen pia inazingatia "hatua ya tano na sita", alisema Sayyid Abdul Malik al-Houthi katika hotuba ya televisheni jana Alhamisi.

Kiongozi wa harakati ya Ansarullah amesisitiza kuwa: "Meli ya kampuni yoyote inayohusika na usambazaji au kusafirisha bidhaa kwa adui Mzayuni italengwa bila ya kujali inaelekea wapi. Meli yoyote inayosafirisha bidhaa kwenye bandari za adui itakuwa shabaha yetu popote mikono yetu itakapofika." 

Harakati ya Ansarullah imekuwa ikilenga meli zenye uhusiano na Israel katika Bahari Nyekundu na Ghuba ya Aden ili kuonyesha  mshikamano na Wapalestina wanaoendelea kuuawa kikatili na majeshi ya Israel. Ansarullah inasema operesheni hizo zitaendelea hadi pale Israel itakaposimamisha vita na mzingiro wake kwenye Ukanda wa Gaza.

Al Houthi amesisitiza kuwa vikosi vya Ansarullah pia vitaendelea kushambulia meli za Marekani na Uingereza zenye uhusiano na adui, Israel.

Al Houthi: Tutaendelea kushambulia meli zenye uhusiano na Israel

Amesema, tangu kuanza kwa operesheni za Ansarullah, meli 112 zimeshambuliwa na kuongeza kuwa, makombora 10 ya balestiki na ndege kadhaa zisizo na rubani zilirushwa kulenga meli za adui katika wiki moja iliyopita.

Tags