Dec 22, 2020 07:34 UTC
  • Hizbullah: Shahidi Suleimani alikuwa nguvu kubwa mbele ya njama za ubeberu wa Marekani

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, shahidi Qassem Suleimani alikuwa nguvu kubwa mbele ya mipango kiistikbari ya Marekani na ndio maana ameuliwa kigaidi na adui.

Akizungumza na tovuti ya habari ya al Ahad katika kukaribia maadhimisho ya kumbukumbu ya kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Suleimani Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH), Sheikh Naim Qassim Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema: nafasi na ushindi wa mhimili wa muqawama uliodhihirishwa na shahid Qassem Suleimani vimemfanya apate nafasi adhimu mbele ya wananchi.  

Shahid Luteni Jenerali , Qassem Suleimani  

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa: kwa kujitolea kundi hilo la muqawama litaendeleza njia yake, na kwamba Hizbullah itakuwa tayari kupigana vita kwa nguvu zote na kuandaa suhula zote za kimlingano kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi ya Israel na uvamizi wake. 

Kamanda Luteni Jenerali shahid Qassem Suleimani ambaye tarehe tatu Januari mwaka huu alielekea Baghdad Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo; aliuliwa shahidi pamoja na Abu Mahdi al Muhandes Naibu Mkuu wa Harakati ya al Hashdu Sha'abi ya Iraq na wanajihadi wenzao 8 katika shambulio la anga la wanajeshi vamizi na magaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad. 

Tags