Nov 04, 2021 23:55 UTC
  • UNRWA: Nusu ya watoto wa Ukanda wa Ghaza wanahitaji msaada wa kisaikolojia

Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetangaza kuwa nusu ya watoto wa Kipalestina wanaoishi katika Ukanda wa Ghaza wanahitaji msaada wa kisaikolojia kutokana athari za vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo hilo.

Thomas White ambaye alishika hatamu za uongozi mwezi Agosti mwaka huu amesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa, baada ya uchunguzi uliofanywa kuhusu wakimbizi wa Kipalestina huko Ghaza imebainika kuwa taathira na matatatizo ya kisaikolojia hasa miongoni mwa watoto wa eneo hilo yameongezeka pakubwa.  

White ameongeza kuwa, vita vya karibuni vya Israel dhidi ya Ghaza vimevuruga ustawi wa kiuchumi katika eneo hilo ambao ulitabiriwa kustawi na kuongezeka kwa asilimia tatu mwaka huu. 

Kwa sasa watoto wa Kipalestian elfu 9,090 wanasumbuliwa na matatizo mbalimbali ya kiakili na madhara waliyopata kutokana na vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel. Amesema watoto hao sasa wanahitaji msaada wa kisaikolojia. 

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina huko Ghaza pia limeweka wazi maafa yaliyozikumba nyumba za familia za wakimbizi wa Kipalestina karibu 8,300 ambazo zimebomolewa kikamilifu au kupata madhara.  

Nyumba za wakimbizi wa Kipalestina huko Ghaza zilizobomolewa katika vita vya Israel 

 

Tags