-
Nasrullah: Siku ya kuuawa shahidi Kamanda Soleimani, mwanzo wa historia mpya Mashariki ya Kati + Video
Jan 05, 2020 12:26Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, tarehe 3 Januari 2020 ambayo ni siku ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, ni mwanzo wa historia mpya katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Mwili wa shahidi Qassem Soleimani na ya mashahidi wenzake yasindikizwa na kuagwa Ahvaz na Mashhad + Video
Jan 05, 2020 12:10Mwili wa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na ya mashahidi wenzake waliouliwa shahidi pamoja naye katika jinai ya kinyama iliyofanywa na majeshi ya kigaidi ya Marekani imesindikizwa na kuagwa leo katika mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mwa Iran na huko Ahvaz kusini mwa nchi.
-
SAUTI, Fadhil Al-Nusr Muhadhiri Chuo Kikuu Tanzania: Qassem Soleimani hakuwa tu kamanda wa kijeshi bali alikuwa mlezi mkubwa wa kiroho
Jan 03, 2020 12:42Dunia imeendelea kutoa radiamali yake kutokana na kuuawa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) Meja Jenerali Qassem Solaimani aliyeuawa shahidi kigaidi na helikopta ya kijeshi ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa mjini Baghdad nchini Iraq mapema leo asubuhi.
-
SAUTI, Mansour Amr wa Kongo DR: Qassem Soleimani alikuwa zaidi ya makamanda duniani, hakusema kwa maneno bali kwa vitendo
Jan 03, 2020 11:16Dunia imegubikwa na huzuni kubwa ya kuuawa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) Meja Jenerali Qassem Solaimani aliyeuawa shahidi kigaidi na helikopta ya kijeshi ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa mjini Baghdad nchini Iraq mapema leo asubuhi.
-
SAUTI, Shirika la Kutetea haki za Wafungwa nchini Burundi NDABARIZA lataka msamaha wa Rais Nkurunziza utekelezwa haraka
Jan 02, 2020 13:32Shirika la Kutetea Haki za Wafungwa nchini Burundi (NDABARIZA), limevitaka vyombo husika vya serikali kutekeleza agizo la Rais Pierre Nkurunziza la kuwaachilia huru wafungwa waliopewa msamaha na rais huyo.
-
Waislamu Zanzibar wahimizwa kujifunza elimu ya ndoa ili kuepuka talaka holela + Sauti
Dec 27, 2019 12:20Waislamu visiwani Zanzibar hasa vijana wametakiwa kulipa umuhimu suala la elimu ya ndoa ili kupunguza wimbi la talaka za kiholela ambazo kimsingi zinahesabiwa ni sehemu moja ya kukanyaga haki za watoto. Hayo na mengineyo yamo kwenye ripoti ya kila wiki ya matukio ya Kiislamu, Afrika Mashariki, kama inavyoletwa kwenu na mwandishi wetu wa Zanzibar, Harith Subeit.
-
Hali ya utulivu yarejea Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya mapigano + Sauti
Dec 27, 2019 12:18Hali ya utulivu imerejea katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui baada ya siku mbili za mapigano baina ya makundi mawili hasimu. Mapigano hayo yamesababisha zaidi ya watu 30 kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Mossi Mwasi na maelezo zaidi…
-
Uganda yapongezwa na WHO kwa kukazania afya ya jamii + Sauti
Dec 27, 2019 12:15Serikali ya Uganda imepongezwa kwa kusimamia na kukazania vyema afya katika jamii kuanzia mashinani. Pongezi hizo zimetolewa na Shirika la Afya Duniani, WHO. Kigozi Ismail na maelezo zaidi kutoka Kampala…
-
Hamas: Utawala wa Kizayuni ndio utakaobeba dhima ya lolote litakalotokea + Video
Dec 26, 2019 08:23Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema kuwa, utawala wa Kizayuni ndio utakaobeba dhima ya lolote litakalotokea kutokana na mashambulizi yake ya mara kwa mara katika Ukanda wa Ghaza.
-
Waziri wa zamani wa DRC ataka Rwanda ivamiwe na kugeuzwa mkoa ili mashariki mwa DRC kuwe salama + Sauti
Dec 25, 2019 07:14Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Adolphe Muzito amesema kuwa, njia pekee ya kumaliza uasi mashariki mwa nchi hiyo ni kuivamia nchi jirani ya Rwanda na kuigeuza kuwa mkoa wa DRC. Mossi Mwasi na maelezo zaidi.