-
Katibu Mkuu wa UN awasili Congo DR kujadili njia za kukabiliana na Ebola + Sauti
Aug 31, 2019 08:48Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewasili katika mji wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wa Goma kwa shabaha ya kutathmini na kuchunguza njia za kukabiliana na ugonjwa hatari wa Ebola.
-
Safari za meli baina ya Kigoma Tanzania na Bujumbura Burundi zaanza tena baada ya miaka 15 + Sauti
Aug 30, 2019 12:22Njia ya usafiri ya "Central Corridor" imezinduliwa rasmi kwa meli ya kwanza tangu miaka 15 kufika katika bandari ya Bujumbura Burundi kutokea Kigoma Tanzania, baada ya meli hiyo kusafirishwa kwa reli kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma. Hamida Issa na maelezo zaidi kutoka Bujumbura.
-
Kesi mpya ya Ebola yagunduliwa nchini Uganda + Sauti
Aug 30, 2019 12:14Wizara ya Afya ya Uganda imesema kuwa msichana mmoja mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amepatikana na virusi vya Ebola nchini Uganda. Wizara hiyo imesema kuwa, msichana huyo mwenye umri wa miaka 9, aliwasili nchini Uganda akitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ingawa hata hivyo haikumtaja jina lake.
-
Matukio ya ulimwengu wa Kiislamu na Harith Subeit + Sauti
Aug 30, 2019 12:11Wiki hii pia kama ilivyo kwa wiki zote, ukanda wa Afrika Mashariki na Kati umeendelea kuwa na matukio mengi ya Kiislamu. Mwandishi wetu wa Zanzibar Harith Subeit anatudondolea baadhi yake katika ripoti yake hii...
-
Burundi na DRC zahimiza ushirikiano mkubwa zaidi baina yao + Sauti
Aug 28, 2019 02:31Meya wa jiji la Bujumbura na mkuu wa jimbo la kivu kusini mashariki mwa DRC wameafikiana kuimarisha ushirikiano ili kukabiliana na makundi ya watu wenye kubebelea silaha wanao hatarisha usalama mara kwa mara katika nchi hizi 2. Pia kuimarisha vita dhidi ya ugonjwa wa Ebola
-
Sheikh Hemen Jalala alalamikia unyanyasaji wa Waislamu Tanzania + Sauti
Aug 26, 2019 02:25Mkuu wa chuo cha kiislamu cha Imam Swadiq AS kilichopo jijini Dar es Salaam Tanzania, Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa kitendo cha kuwatilia shaka Waislamu wa kwa sababu ya kwenda nchi za Iran, Iraq, Syria, Saudi Arabia na Lebanon, ni kuvunja uhuru wao wa ibada. Ammar Dachi na maelezo zaidi...
-
Mufti wa Zanzibar awataka wanawake wa Kiislamu kuwa mstari wa mbele kutetea dini yao + Sauti
Aug 26, 2019 02:02Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh al Kaabi, amewataka wanawake wa Kiislamu visiwani humo kuwa mstari wa mbele katika kutetea dini yao. Harith Subeit na maelezo zaidi kutoka Zanzibar...
-
Makubaliano ya kukomesha uhasama baina ya Uganda na Rwanda
Aug 23, 2019 01:40Siku moja baada ya Uganda na Rwanda kusaini makubaliano ya kukomesha matatizo yao, baadhi ya wachambuzi wanasema makubaliano hayo yaliyosainiwa Luanda Angola yatakuwa na maana ikiwa yatatekelezwa. Sylvanua Karemera na maelezo zaidi kutoka Kigali...
-
Magari yanayotumia gesi yaongezeka nchini Tanzania
Aug 23, 2019 01:34Serikali ya Tanzania imebainisha kuwa matumizi ya gesi asilia katika magari yamezidi kukua nchini humo ambapo kwa sasa idadi ya magari hayo imefikia 210 kutoka 65 yaliyokuwa yakitumia nishati hiyo mwaka 2017. Mwandishi wetu Ammar Dachi ana maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam....
-
Video inayowaonesha wanajeshi wa SEPAH wa Iran wakiionya manuwari ya kivita vya Uingereza isiingilie operesheni ya kuzuia meli ya mafuta ya nchi hiyo
Jul 29, 2019 16:18Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH limesambaza mkanda wa video na sauti wakati jeshi hilo lilipotoa onyo kwa Manuwari ya Kifalme wa Uingereza kwamba ikae mbali na isiingilie operesheni ya kusimamishwa meli ya mafuta iliyokuwa inapeperushwa bendera ya Uingereza katika eneo la Ghuba ya Uajemi.