-
Umoja wa Mataifa walaani vikali shambulio na utekaji nyara wanafunzi Nigeria
Feb 19, 2021 10:25Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kupitia msemaji wake, amelaani vikali shambulio la tarehe 17 Februari mwaka huu 2021 dhidi ya Chuo cha Sayansi cha serikali cha Kagara katika mkoa wa kaskazini kati mwa Nigeria.
-
Mabaharia wa Uturuki waliotekwa nyara Nigeria warejea nyumbani
Feb 14, 2021 09:27Mabaharia 15 wa Uturuki waliotekwa nyara mwezi uliopita katika Ghuba ya Guinea wamerejea nyumbani leo Jumapili huku nahodha wao akisema walikabiliwa na vitisho vya kuuawa wakati waliposhikiliwa kwa muda wa wiki tatu msituni.
-
Makumi wauawa katika hujuma za wabeba silaha Nigeria
Feb 10, 2021 20:04Makumi ya watu wameuawa katika mashambulizi kadhaa ya magenge ya wabeba silaha katika wilaya tano za eneo la kaskazini magharibi mwa Nigeria.
-
Amnesty yasema Nigeria inajaribu kuficha mauaji ya raia mjini Lagos
Jan 29, 2021 04:16Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeituhumu serikali ya Nigeria kuwa inafanya jitihada za kuficha mauaji ya kutisha ya wananchi waliokuwa wakiandamana katika mji wa Lagos mwezi Oktoba mwaka uliopita.
-
Kuakhirishwa kesi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky nchini Nigeria
Jan 28, 2021 22:34Katika hali ambayo Waislamu nchini Nigeria wameshiriki katika maandamano ya amani ya kutaka kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, mwendesha mashtaka mkuu nchini humo ameakhirisha tena kesi ya kiongozi huyo wa harakati ya Kiislamu.
-
ISIS yadai kuhusika na kutekwa kambi ya jeshi Nigeria
Jan 17, 2021 04:30Maafisa usalama na mamia ya wakazi wa mji mmoja katika jimbo la Borno la kaskazini mwa Nigeria wamelazimika kuyakimbia makazi yao baada ya genge la magaidi waliojizatiti kwa silaha kushambulia na kudhibiti kambi ya jeshi katika eneo hilo.
-
Shambulio la bomu la Boko Haram laua askari 11 Nigeria
Dec 30, 2020 11:25Maafisa usalama 11 wakiwemo wanajeshi wanne wameuawa katika shambulio la bomu la kutegwa ardhini la kundi la kigaidi la Boko Haram katika jimbo la Borno huko kaskazini mashariki mwa Nigeria.
-
Magaidi wa Boko Haram wateka nyara makumi ya wakata mbao Nigeria
Dec 27, 2020 11:58Magaidi wakufurishaji wa kundi la Boko Haram wamewateka nyara wakata mbao zaidi ya 40 na kuwaua wengine watatu katika jinai yao ya hivi karibuni.
-
Boko Haram yashambulia vijiji kadhaa na kuua katika mkesha wa Krismasi
Dec 25, 2020 10:09Watu saba wameuawa huku wengine wengi wakijeruhiwa baada ya kundi la kigaidi la Boko Haram kushambulia vijiji kadhaa katika majimbo ya Borno na Adamawa nchini Nigeria, usiku wa kuamkia leo.
-
Wananchi wa Nigeria waandamana kuiunga mkono Palestina na kupinga kuanzishwa uhusiano na Israel
Dec 21, 2020 23:27Wananchi wa Nigeria wameandamana na kutangaza uungaji mkono wao kwa taifa la Palestina na kupinga harakati za baadhi ya mataifa ya Kiarabu za kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.