-
Benki ya ADB yaridhishwa na miradi yake Burundi + Sauti
Feb 07, 2019 14:21Ujumbe wa Benki ya Mandeleo ya Afrika ADB baada ya ziara yake ya wiki moja nchini Burundi umesema kuwa umeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyodhaminiwa na benki hiyo nchini humo. Hamida Issa na maelezo zaidi kutoka Bujumbura...
-
Wazazi Njombe Tanzania walazimika kuacha kazi na kusindikiza watoto shuleni wasiuawe + Sauti
Feb 03, 2019 14:33Wazazi mkoani Njombe nchini Tanzania wameongeza uangalifu kwa watoto wao na wengine wanaacha shughuli zao ili kusindikiza watoto wao shuleni. Hii ni kutokana na wimbi la mauaji ya watoto hao mkoani humo. Amari Dachi na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam...
-
EAC inayoendelea na kikao mjini Arusha Tanzania, yalaumiwa + Sauti
Feb 02, 2019 04:43Kikao cha siku mbili cha 20 cha kawaida cha wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC kinachofanyika mjini Arusha Tanzania, jana Ijumaa, Februari Mosi 2019 kilimteua Rais Paul Kagame wa Rwanda kuwa mwenyekiti wake mpya baada ya kumalizika uenyekiti wa kupokezana wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda. Hata hivyo jumuiya ya Afrika Mashariki inalaumiwa kwa kutotekeleza kivitendo maazimio mengi inayofikia kwenye vikao vyake. Kigozi Ismail na maelezo zaidi kutoka Kampala...
-
Kampeni ya kusafisha majambazi yaendelea nchini Uganda + Sauti
Jan 29, 2019 23:49Maafisa usalama nchini Uganda wamewatia mbaroni majambazi kadhaa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala na viunga vyake. Majambazi hao wanatuhumiwa kufanya vitendo mbalimbali vya uhalifu na uvunjaji sheria ikiwa ni pamoja na mauaji na kuwateka nyara watoto wadogo. Kigozi Ismail na maelezo zaidi kutoka Kampala...
-
Kikao cha Burundi chahimiza kupunguzwa athari za majanga ya kimaumbile + Sauti
Jan 28, 2019 23:04Wajumbe wanaoshiriki katika kikao cha nchi za Afrika ya Kati cha Bujumbura Burundi wamehimiza kuchukuliwa hatua za kukabiliana na athari za majanga ya kimaumbile na ugonjwa hatari wa Ebola uliopinga kambi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hamida Issa na maelezo zaidi kutoka Bujumbura...
-
MONUSCO yatuma askari zaidi katika kijiji cha Yumbi DRC + Sauti
Jan 28, 2019 23:00Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO umetuma askari zaidi katika kijiji cha Yumbi mkoani Maindombe, kaskazini magharibi mwa mji mkuu Kinshasa mahali palipotokea mapigano ya kikabila mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka jana. Mossi Mwassi na maelezo zaidi...
-
Viongozi wa dini Tanzania: Kubeti ni kamari, ni haramu! + Sauti
Jan 27, 2019 14:50Viongozi wa kidini na wa kiserikali nchini Tanzania wamekemea vitendo vya kubeti na kucheza kamari ambavyo vimekithiri nchini humo hali ambayo inapelekea kuzalika vijana wasiofanya kazi wakiweka matumaini zaidi ya kupata kipato chao kupitia njia hizo. Ammar Dachi na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam Tanzania.
-
Waislamu Kenya walalamikia marufuku ya Hijabu mashuleni + Sauti
Jan 24, 2019 13:16Waislamu nchini Kenya wamelalamikia uamuzi wa Mahakama ya Kilele ya nchi hiyo wa kubatilisha ruhusa ya wanafunzi wa kike kuvaa vazi la staha la Hijabu katika shule zote za nchi hiyo. Seifullah Murtadha na maelezo zaidi...
-
Burundi: Kuna njama za kuvuruga uhusiano wetu na Tanzania + Sauti
Jan 21, 2019 14:51Mashirika ya Capes na Pisc ya nchini Burundi yamesema kuwa, kugunduliwa sare za jeshi la Tanzania katika kambi ya wakimbizi huko Burundi kunadhihirisha kuwepo njama za kutaka kuvuruga uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili. Hamida Issa na maelezo zaidi kutoka Bujumbura.
-
Washukiwa wanne wa ugaidi wajisalimisha nchini Kenya + Sauti
Jan 21, 2019 14:46Washukiwa wanne kati ya wanane waliokuwa wakisakwa na mamlaka za usalama nchini Kenya wamejisalimisha huku polisi wakizidisha msako kote nchini humo.