Aug 03, 2023 02:46 UTC
  • Ripoti: Wapalestina zaidi ya 200 wameuawa shahidi tangu kuanza mwaka huu

Vikosi vya usalama vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimewaua shahidi Wapalestina zaidi ya 200 tangu kuanza mwaka huu 2023.

Ripoti mpya imeeleza kuwa, utawala huo haramu umewaua shahidi Wapalestina 212 wasio na hatia yoyote tokea Januari mwaka huu hadi sasa katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Utawala huo pandikizi unawaua shahidi Wapalestina wakiwemo watoto wadogo na wanawake wasio na hatia kila uchao mkabala wa kimya cha jamii ya kumataifa.

Aidha ripoti mpya iliyotolewa na kituo cha kutetea maslahi ya wafungwa wa Palestina cha PCPS imesema maafisa usalama wa utawala wa Kizayuni wamewatia mbaroni mamia ya watoto wa Kipalestina tokea mwanzoni mwa mwaka huu hadi sasa.

 

Katika upande mwingine, ripoti ya Umoja wa Mataifa imebaini kuwa, mwezi uliopita wa Julai pekee vikosi vya kijeshi vya utawala haramu wa Israel vilibomoa majengo 54 yanayomilikiwa na Wapalestina huko Quds (Jerusalem) Mashariki katika tarafa kubwa zaidi ya eneo la Ukingo wa Magharibi eneo linalokaliwa kwa mabavu.

utawala haramu wa Israel mara kwa mara hubomoa nyumba za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds Mashariki inayokaliwa kwa mabavu, kwa madai kuwa majengo hayo yamejengwa bila vibali, jambo ambalo linapingwa vikali na wananchi wa Palestina.

Tags