Damascus: Marekani imefanya uhalifu mpya dhidi ya jeshi la Syria
Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetangaza kuwa Marekani imezidisha vitendo uhalifu na jinai mpya za katika nchi hiyo.
Ni baada ya chanzo cha usalama kutangaza Ijumaa iliyopita kuwa wanajeshi 20 wa Syria waliuawa na wengine 10 kujeruhiwa katika shambulizi dhidi ya basi lililokuwa limewabeba katika viunga vya mashariki mwa Deir Ezzor mashariki mwa Syria.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetangaza kuwa, vikosi vamizi vya Marekani vimefanya jinai mpya na kushambulia basi lililokuwa limebeba askari wa jeshi la Syria kusini-mashariki mwa Deir Ezzor, vikishirikiana na makundi ya kigaidi na kuua askari kadhaa.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria inasema: Hujuma hiyo ya kigaidi inalenga kuzidisha harakati za Marekani dhidi ya mamlaka, uhuru na ardhi ya Syria na kuyasaidia makundi ya kigaidi hususan kundi la kigaidi la ISIS, na vilevile kuwatumia wanamgambo wanaotaka kujitenga kama chombo cha utekelezaji wa mipango yake nchini Syria na magharibi mwa Asia kwa ujumla.
Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria, imeeleza kuwa: Damascus inasisitiza azma yake ya kupambana na magaidi ili kuangamiza mabaki ya makundi hayo na itaendeleza jiitihada za kukomboa ardhi yake kutoka kwenye uvamizi Marekani, utawala haramu wa Israeli na Uturuki kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Majeshi ya Marekani yanakalia kwa mabavu maeneo yenye utajiri wa mafuta ya mashariki na kaskazini mashariki mwa Syria. Marekani inaendelea kuyakalia kwa mabavu maeneo hayo kwa kisingizio cha kupambana na ISIS.