Jun 29, 2016 07:48 UTC
  • Siku ya Quds, Siku ya kuikomboa Baitul Muqaddas

Idadi kadhaa ya wanazuoni na wanasiasa wa Ulimwengu wa Kiislamu wameitaja Siku ya Kimataifa ya Quds kuwa ni Siku ya kuikomboa Baitul Muqaddas na kuwaunga mkono waliodhulumiwa.

Muhammad al Auni Mkuu wa Taasisi ya Kutetea Uhuru wa Kujieleza nchini Morocco amesema kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ni fursa kwa ajili ya kutoa mwito kwa ulimwengu mzima wa kuikomboa Quds Tukufu na Palestina inayokaliwa kwa mabavu kutoka katika makucha ya Wazayuni.

Naye Sheikh Muhammad Hussein Mufti Mkuu wa Quds na Palestina amesema kuwa Waislamu wote na wananchi wa nchi za Kiarabu na serikali zao wanapasa kutekeleza jukumu lao katika kutetea Msikiti wa al Aqsa kibla cha kwanza cha Waislamu.

Ahmad al Sahn Mkurugenzi wa habari wa televisheni ya Iraq ya al Tijah pia amesema kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ni Siku ya uadilifu na usawa na ni siku ya kuzungumzia kadhia kuu ya Palestina katika fikra za Umma wa Kiislamu. Hisham Salem Katibu Mkuu wa Harakati ya Palestina ya as-Swabirin amesema katika Siku ya Kimataifa ya Quds, Waislamu wote wanapasa kuonyesha hasira zao kwa kutawala wa Kizayuni. Hii ni kwa sababu utawala huo unatekeleza siasa za mauaji na kuwazingira wananchi madhlumu wa Palestina, unatenda jinai na hujuma mbalimbali dhidi ya raia hao wasio na hatia. Itakumbukwa kuwa Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani huadhimishwa kila mwaka kama siku ya kimataifa ya Quds.

Tags