Rais wa Syria akosoa misimamo ya kindumakuwili ya Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i10291-rais_wa_syria_akosoa_misimamo_ya_kindumakuwili_ya_magharibi
Rais wa Syria amezikosoa nchi za Magharibi kwa kutekeleza siasa za kindumakuwili kuhusu nchi yake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 30, 2016 08:34 UTC
  • Rais wa Syria akosoa misimamo ya kindumakuwili ya Magharibi

Rais wa Syria amezikosoa nchi za Magharibi kwa kutekeleza siasa za kindumakuwili kuhusu nchi yake.

Akizungumza na televisheni ya SBS ya Australia, Rais Bashar al Assad amekosoa misimamo ya kindumakuwili ya Magharibi kuhusiana kadhia ya nchi yake na kueleza kuwa nchi za Magharibi kwa upande mmoja zinaishambulia kisiasa Syria na katika upande wa pili zinawatuma maafisa wao hususan maafisa wa masuala ya usalama huko Damascus ili kushirikiana na kufanya mazungumzo ya siri na Syria.

Rais Bashar al Assad ameongeza kuwa matamshi yanayokinzana ya viongozi wa Australia na msimamo rasmi wa nchi hiyo kuhusu kadhia ya Syria, kiujumla yote hayo yanadhihirisha wazi misimamo ya kindumakuwili ya nchi za Magharibi.

Rais wa Syria amesisitiza kuwa nchi zote za Magharibi ni vibaraka wa Marekani na kwamba kile kinachoamrishwa na Washington, kinatekelezwa na nchi hizo.