Ansarullah ya Yemen yafanya shambulizi la droni dhidi ya Israel
Harakati ya Ansarullah ya Yemen imefanya mashambulizi dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kutumia ndege zisizo na rubani.
Abdelaziz bin Habtour, Waziri Mkuu wa Serikali ya Ansarullah ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, "droni hizo ni milki ya dola la Yemen."
Vyombo vya habari vya Wazayuni vimethibitisha habari ya kufanyika shambulizi hilo la droni ambalo limepelekea anga ya ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu kuhinikiza kwa sauti za ving'ora.
Vyombo hivyo vimedai kuwa, utawala wa Kizayuni umeharibu 'shabaha' ya kitu kisichojulikana katika anga ya Bahari Nyekundu.
Wazayuni katika eneo la kitalii la Eilat wameingiwa na kiwewe na wameonekana wakikimbia huku na kule baada ya kufanyika shambulizi hilo la droni la Ansarullah.
Utawala haramu wa Israel umedai kuwa shambulizi hilo halijakuwa na hatari kwa eti raia na kwamba droni hizo zilitoka kaskazini mwa Yemen, eneo ambalo linadhibitiwa na wanamuqawama wa Houthi.
Ansarullah imesema imefanya shambulizi hilo la ndege zisizo na rubani kujibu jinai za Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza. Israel ilianzisha vita vyake vya umwagaji damu kwenye Ukanda wa Gaza Oktoba 7 baada ya mashambulizi ya kushtukiza, yaliyopewa jina la Kimbunga cha al-Aqsa ya wanamuqwama wa Hamas.
Tangu kuanza vita hivyo, utawala wa Israel umekuwa ukifanya jinai za kivita huko Gaza na kuwaua zaidi ya Wapalestina 8,500 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.