Tel Aviv inataka kuongeza muda wa usitishaji vita
Televisheni ya utawala wa Kizayuni wa Iisrael (Kan) leo Jumatano imetangaza kuwa Israel inafanya jitiada za kurefusha muda wa usitishaji vita baada ya kumaliza siku mbili zilizoongezwa.
Amir Buttershalom, mchambuzi wa masuala ya usalama katika televisheni ya 12 ya Israel ameeleza kuwa: Kuna mapatano kuhusu siku ya saba na nane ya usitishaji vita ambayo yanaonyesha kuwa huwenda usitishaji vita ukarefushwa kwa siku ya 9 na 10.
Mchambuzi huyo wa Israel ameongeza kusema: Tathmini ya viongozi wa Israel inaonyesha kuwa usitishaji vita umeongezwa kwa muda kwa siku mbili nyingine ili kuwaachia huru wafungwa zaidi na baada ya hapo vita vitanza tena mwishoni mwa wiki hii.
Wakati huo huo gazeti la Yedioth Ahronoth limemnukuu kiongozi wa kisiasa wa serikali ya Tel Aviv na kuripoti kuwa:" Iwapo kutakuwa na pendekezo la kuongeza muda wa usitishaji vita kwa zaidi ya siku 10 basi watalichunguza."
Pande za Palestina na Israel Jumatatu usiku wiki hii katika siku ya nne ya usitishaji vita wa awali zilikubaliana kurefusha mapatano hayo huko Ukanda wa Gaza kwa siku mbili nyingine kwa kuzingatia masharti ya awali yaani kusitisha vita, kubadilishana mateka na kuruhusu kuingia misaada ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza.