Nasrullah: Kuuawa shahidi 'ni sehemu ya utamaduni wetu ili kulinda mataifa yetu'
(last modified Fri, 12 Jul 2024 11:32:39 GMT )
Jul 12, 2024 11:32 UTC
  • Sayyid Hassan Nasrullah
    Sayyid Hassan Nasrullah

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah ametilia mkazo wajibu kupambana na kuwa tayari kuuliwa shahidi katika kulinda madola ya Kiislamu dhidi ya uvamizi na kukaliwa kwa mabavu na maadui.

Katika hotuba yake iliyorushwa hewani kwa njia ya televisheni usiku wa kuamkia leo, Sayyid Nasrullah amesema wapiganaji wa harakati hiyo ya Muqawama walikomboa maeneo ya Lebanon kutoka kwenye uvamizi wa Israel, wakalinda heshima na kustawisha maeneo yaliyokombolewa kutokana na utamaduni wa kuwa tayari kufa shahidi.

"Fikra ya mapambano, kusimama kidete na kuwa tayari kuuawa shahidi ni muhimu kwa utamaduni wetu wenye thamani wa maisha, kwa sababu inatuwezesha kulinda mataifa yetu na kulinda utajiri na rasilimali zetu dhidi ya uvamizi na uporaji," amesema Sayyid Nasrullah.

Karbala, Iraq

Kiongozi wa Hizbullah ameshiria vita vya ushindi vya wanamapambano vilivyopiganwa katika historia ya mwanadamu na kusema: "Wavietnamu waliweza kukomboa nchi yao kwa kusimama imara, subira, na mshikamano dhidi ya wavamizi wa Kimarekani." Sayyid Nasrullah alikuwa akiashiria vita vya miaka ya 1960 na 70 vya wapiganaji wa Vietnam dhidi ya Marekani iliyovamia nchi hiyo.

Vilevile ameashiria kusimama kidete kwa taifa la China wakati wa vita dhidi ya Ufalme wa Japani kutoka 1937 hadi 1945 kama sehemu ya Vita vya Pili vya Dunia.

"Kama taifa la China lingesalimu amri, lingelazimika kuendelea kuwa chini ya utawala vamizi," amesisitiza Sayyid Hassan Nasrullah na kuongeza kuwa: "Kama taifa la China lisingepambana yumkini kwamba lingekuwa nchi zaidi kuliko mataifa mengi ya ulimwengu wa tatu. Hata hivyo, limeibuka kama taifa kubwa kimataifa.” 

Amesema, "Wapiganaji wetu waliouawa shahidi wametengeza maisha na ushindi huko Gaza, Lebanon, Yemen, Iraq na kwingineko katika kanda hii, na kinyume chake, Marekani na mshirika wake, Israel zinazoendeleza uharibifu na maafa."

Matamshi hayo ya Katibu Mkuu wa Hizbullah ni sehemu ya hotuba zake za Mwezi wa Muharram katika kumbukumbu ya mapambano ya mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (saw), Imam Hussein bin Ali (as) dhidi ya utawala dhalimu wa Bani Umayyah katika ardhi ya Karbala mwaka 61 Hijria. 

Mwezi uliopita wa Juni pia kiongozi wa kijeshi wa harakati ya Hamas, Yahya Sinwar, alifananisha vita vya Gaza na mapambano ya Imam Hussein (as) huko Karbala.