OIC yalaanii jinai mpya ya Israel na kutaka ilazimishwe kusitisha vita
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i115078-oic_yalaanii_jinai_mpya_ya_israel_na_kutaka_ilazimishwe_kusitisha_vita
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani jinai mpya ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, na kusisitiza kuwa, utawala huo unapaswa kulazimishwa kuanzisha usitishaji vita mara moja.
(last modified 2024-08-11T02:14:07+00:00 )
Aug 11, 2024 02:14 UTC
  • OIC yalaanii jinai mpya ya Israel na kutaka ilazimishwe kusitisha vita

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani jinai mpya ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, na kusisitiza kuwa, utawala huo unapaswa kulazimishwa kuanzisha usitishaji vita mara moja.

Katika taarifa yake jana (Jumamosi), Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu imelaani jinai mpya iliyofanywa na utawala wa Kizayuni katika Shule ya al-Tabieen katika mji wa Gaza ambayo imesababisha kuuawa shahidi zaidi ya watu 100 na kujeruhiwa idadi nyingine ya wakimbizi wa Kipalestina. , na kusema: Uhalifu huu ni mauaji ya halaiki ya wavamizi wa Israel katika Ukanda wa Gaza na ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na amri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki na maazimio husika ya Baraza la Usalama. OIC imebainisha katika taarifa yake hiyo kwamba, Israel iinabeba dhima ya jinai hiyo na kutaka viongozi wa utawala huuo kushtakiwa kwa kutenda jinaii za kivita na jinai dhidi ya binadamu.

Watoto ndio wahanga wakuu wa jinai za Israel huko Gaza

 

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeitaka jamii ya kimataifa hususan Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuulazimisha utawala huo utekeleze majukumu yake kwa mujibu wa sheria za kimataifa na kusitisha vita katika Ukanda wa Gaza.

Jana alfajiri jeshi la utawala vamizi wa Israel lilishambulia kwa bomu shule ya "Al-Tabieen" katika kitongoji cha Al-Daraj baada ya Swala ya Alfajiri na kuua zaidi ya Wapalestina 100.