OIC yatakiwa kuunga mkono mhimili wa muqawama
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i115166-oic_yatakiwa_kuunga_mkono_mhimili_wa_muqawama
Mkuu wa Baraza la Maulamaa wa Nigeria amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Waislamu wa Gaza, ambayo yalisababisha vifo vya watu karibu 200 walipokuwa wakiswali Swala ya alfajiri katika shule ya Tabeen.
(last modified 2024-08-12T23:07:39+00:00 )
Aug 12, 2024 23:07 UTC
  • OIC yatakiwa kuunga mkono mhimili wa muqawama

Mkuu wa Baraza la Maulamaa wa Nigeria amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Waislamu wa Gaza, ambayo yalisababisha vifo vya watu karibu 200 walipokuwa wakiswali Swala ya alfajiri katika shule ya Tabeen.

Sheikh Dan'azumi Musa ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na Shirika la Habari la Iran Press ameitaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kuunga mkono mhimili wa muqawama unaoongozwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na utawala wa kigaidi wa Kizayuni kwa ajili ya ukombozi wa Palestina.

"Sisi, katika Baraza la Maulamaa wa Nigeria, tunalaani shambulio la kinyama na la kikatili la Israel dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza, ambalo hivi karibuni liliua karibu watu 200, alisema.

Nembo za baadhi ya makundi ya muqawama

 

Mwanazuoni huyo mwandamizi wa Kiislamu wa Kisuni wa Nigeria ameongeza kuwa: "Tunaiomba kwa moyo wote jumuiya ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kutoa uungaji mkono wote unaohitajika kwa kambi hii ya Mhimili wa muqawama inayoongozwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambao inajaribu kufanikisha ukombozi wa Palestina na watu wanaodhulumiwa zaidi duniani, hasa watu wa Gaza."

Kadhalika amesema: Vile vile ninawahimiza Waislamu wote duniani kote, sio Nigeria pekee, kuwaunga mkono watu wa Palestina na pia kuunga mkono mhimili wa muqawama unaoongozwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mwenyezi Mungu awape mafanikio ya mwisho ili watu wa Palestina wapate ushindi kwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu.