Aug 27, 2024 02:12 UTC
  • Watoto wa Kipalestina wanasumbuliwa na utapiamlo mkali huko Gaza

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa maelfu ya watoto katika Ukanda wa Gaza wanasumbuliwa na utapiamlo mkali kutokana na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katka eneo hilo na kuzuiwa bidhaa za chakula kuingia katika eneo hilo.

Shirika la WHO limeashiria mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na kuzuia kuingizwa bidhaa za chakula katika eneo hilo na kusema, watoto karibu 3,200 wa Kipalestina wana hali mbaya kutokana na utapiamlo mkali.  

Hospitali ya Kamal Adwan inayotoa huduma huko Gaza chini ya usimamizi wa Shirika la Afya Duniani imetangaza kuwa watoto wa Kipalestina karibu elfu tano wana dalili za utapiamlo na kwamba ni lazima wapate huduma na msaada wa kitiba.

Watoto wa Kipalestina na tatizo la utapiamlo 

Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo ametahadharisha kuwa tatizo la utapiamlo katika Ukanda wa Gaza limepelekea watoto walioathiriwa kufikia hatua hatari, jambo ambalo linaweza kuwafanya wafariki dunia kwa sababu ya njaa.  

Tags