Radiamali ya Nicaragua kwa mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni huko Palestina na Lebanon
(last modified Tue, 01 Oct 2024 06:18:26 GMT )
Oct 01, 2024 06:18 UTC
  • Radiamali  ya Nicaragua kwa mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni huko Palestina na Lebanon

Valdrack Jaentschke Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Nicaragua amekosoa vikali na mfumo usio wa haki unaotawala dunia hivi sasa na kulaani vikali mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni na waitifaki wake dhidi ya watu madhulumu wa Palestina na Lebanon.

Kwa mujibu wa shirika la habari la  IRNA, Waziri wa Mambo ya Nje wa Nicaragua Valdrack Jaentschke amekosoa vikali  utaratibu huo wa sasa usio wa haki unaotawala dunia na juhudi za kimfumo za madola ya kikoloni na kibeberu kuharibu utamaduni na haki za mataifa mengine.

Aidha amelaani hatua za madola makubwa ulimwenguni dhidi ya Nicaragua na nchi rafiki zikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Cuba, Syria na Venezuela.

Nicaragua imelaani vikali  mauaji ya halaiki ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Palestina na Lebanon

Kikao cha 79 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA)  kilichoanza Jumanne mwezi  Septemba tarehe 24 kwa kuhudhuriwa na wakuu wa nchi mbalimbali mjini New York Marekani  kilimalizika Jumatatu ya jana.