UNRWA: Kizazi kizima cha Wapalestina kitanyimwa haki ya elimu Gaza
Philippe Lazzarini, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), ameonya kuwa, kizazi kizima cha Wapalestina huko Gaza "kitanyimwa haki ya elimu" ikiwa asasi hiyo katika Ukanda huo itafutwa chini ya sheria mpya ya Israel.
Knesset (bunge) ya utawala wa Kizayuni ilipitisha sheria dhidi ya UNRWA wiki iliyopita kwa kuidhinishwa na wawakilishi 92 dhidi ya upinzani wa wawakilishi 10, ambayo inapiga marufuku shughuli za UNRWA katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na utawala huo pandikizi tangu mwaka 1948.
Kamishna Mkuu wa UNRWA anaonya kwamba, endapo sheria ya kupiga marufuku shughuli za UNRWA itatekelezwa basi kutatokea maafa makubwa yakiwemo katika sekta ya elimu.
Lazzarini ameongeza kusema kuwa, kwa kukosekana kwa utawala wa serikali au serikali yenye uwezo, ni UNRWA pekee ambayyo inaweza kutoa elimu kwa wasichana na wavulana zaidi ya 660,000 kote Gaza Amesisitiza kuwa, kwa kukosekana kwa UNRWA, kizazi kizima kitanyimwa haki ya elimu.
Wakati huo huo, chi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimetakiwa kuzuia kutekelezwa sheria zilizopitishwa na bunge la Israel za kupipiga marufuku shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA.