Yemen yaonya Marekani, Israel: 'Kinachokuja ni kikubwa zaidi' 
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i124176-yemen_yaonya_marekani_israel_'kinachokuja_ni_kikubwa_zaidi'
Harakati ya muqawama ya watu wa Yemen, Ansarullah, imeapa kwamba nchi hiyo itaongeza operesheni zake dhidi ya ngome za Marekani na Israel ili kujibu uchokozi wa Marekani dhidi ya ardhi ya Yemen na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina hasa mzingiro na mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza. 
(last modified 2025-03-21T04:31:15+00:00 )
Mar 21, 2025 04:31 UTC
  •  Yemen yaonya Marekani, Israel: 'Kinachokuja ni kikubwa zaidi' 

Harakati ya muqawama ya watu wa Yemen, Ansarullah, imeapa kwamba nchi hiyo itaongeza operesheni zake dhidi ya ngome za Marekani na Israel ili kujibu uchokozi wa Marekani dhidi ya ardhi ya Yemen na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina hasa mzingiro na mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza. 

Ali al-Qahoum, mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya Ansarullah, alitoa matamshi hayo Alhamisi, akionya kwamba Marekani na utawala wa Kizayuni zinapaswa kujiandaa kwa operesheni kali zaidi kutoka Yemen.

Afisa huyo ametangaza utayari wa Yemen wa kukabiliana na maadui wanaoilenga nchi hiyo huku akisisitiza nguvu na uwezo mkubwa wa ulinzi wa taifa hilo, na kuonya, "kinachokuja ni kikubwa zaidi." 

Amesisitiza tena kuwa Yemen itaendelea kuwasaidia Wapalestina hasa katika Ukanda wa Gaza , akibainisha kwamba uungaji mkono huo utaendelea hadi mzingiro na vita vikome

Vikosi vya Jeshi la Yemen mara kwa mara hushambulia meli za kivita  za Marekani zilizoko nje ya pwani ya nchi hiyo.

Vikosi hivyo vya Yemen vilienga uwanja wa ndege wa utawala wa Israel, Ben Gurion, kwa kombora la hypersonic aina ya Palestina-2 hapo jana, ikiwa ni sehemu ya mashambulizi ya kuunga mkono Palestina

Jeshi la Yemen pia jana lilirusha kombora la hypersonic dhidi ya kituo cha kijeshi kusini mwa mji unaokaliwa kwa mabavu wa Yaffa, karibu na Tel Aviv.

Msemaji Mkuu wa Jeshi Brigedia Jenerali Yahya Saree amesisitiza kwamba operesheni hizo, pamoja na zile zinazotekelezwa kwenye njia muhimu za baharini zinazotumiwa na utawala wa Israeli, zitaendelea hadi uchokozi dhidi ya Gaza utakapositishwa sambamba na kuondolewa mzingiro wa utawala huo kwenye ardhi ya Palestina.