Makumi ya wabunge duniani waitaka Israel ikome kuwaadhibu kwa kiu na njaa Wapalestina
(last modified Fri, 23 May 2025 02:59:40 GMT )
May 23, 2025 02:59 UTC
  • Makumi ya wabunge duniani waitaka Israel ikome kuwaadhibu kwa kiu na njaa Wapalestina

Makumi ya wabunge kote duniani wametoa taarifa wakitaka hatua za haraka zichukuliwe kukomesha njaa katika Ukanda wa Ghaza.

Makumi ya wabunge hao wamesema katika taarifa yao kuwa: Mzingiro mkali uliowekwa na utawala wa Israel tangu Oktoba 7, 2023 ambao umeshika kasi zaidi katika wiki za hivi karibuni na kusababisha uhaba mkubwa wa chakula, dawa na mafuta, unawaweka Wapalestina zaidi ya milioni mbili kwenye baa la njaa na kutishia maisha yao.

Tunataka kufunguliwa tena mara moja na bila ya masharti vivuko vyote kuingia Ghaza, pamoja na kivuko cha Rafah.

Taarifa hiyo imeendelea kuksema: "Pia tunatoa mwito kwa pande zote kuondoa vikwazo vyote vya kuingia misaada ya kibinadamu, chakula, mafuta, maji na dawa huko Ghaza."

Taarifa hiyo imeongeza: "Tunasisitizia haja ya kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu unalindwa na kuwezesha shughuli zao kutendeka kwa usalama na amani hadi mashinani."

Taarifa hiyo inahitimisha kwa kusema: "Tunatoa mwito wa kuweko ufuatiliaji wa kimataifa ili kuhakikisha sheria za kimataifa za kibinadamu zinaheshimiwa na utawala wa Kizayuni unapigwa marufuku kutumia njaa kama silaha ya kivita."