Amnesty International imetaka Israel iwekewe vikwazo haraka iwezekanavyo
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i131080-amnesty_international_imetaka_israel_iwekewe_vikwazo_haraka_iwezekanavyo
Shirika la Amnesty International limeitaka jamii ya kimataifa kuiwekea Israel vikwazo haraka iwezekanavyo kutokana na vita na mauaji ya kimbari yanayoendelea kutekelezwa na utawala huo katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2025-09-21T11:03:59+00:00 )
Sep 21, 2025 11:03 UTC
  • Amnesty International imetaka Israel iwekewe vikwazo haraka iwezekanavyo

Shirika la Amnesty International limeitaka jamii ya kimataifa kuiwekea Israel vikwazo haraka iwezekanavyo kutokana na vita na mauaji ya kimbari yanayoendelea kutekelezwa na utawala huo katika Ukanda wa Gaza.

Agnes Callamard Katibu Mkuu wa Shirika la Amnesty International ameiambia televisheni ya al Jazira kwamba mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza yasingewezekana bila ushiriki na msaada wa nchi, taasisi na makampuni mbalimbali.

Amesema maelfu ya makampuni duniani yameiunga mkono Israel moja kwa moja na hivyo kurefusha vita ya tawaa huo dhidi ya Gaza. 

Bi Callamard ameeleza kukaliwa kwa mabavu mji wa Gaza kuwa ni jinaii yeney lengo la kufuta utamaduni na historia ya Wapalestina kupitia kuwafurisha katika ardhi zao. 

Israel inapasa kuwekewa mara moja vikwazo vya kiuchumi na kulaani tu jinai za utawala huo kwa maneno hakutoshi. 

Katibu Mkuu wa Amnesty International amebainisha haya huku mashinikizo ya kimataifa dhidi ya Israel yakiongezeka. 

Alon Ben David mchambuzi wa masuala ya kijeshi wa Kanali ya 13 ya Israel alikiri hivi karibuni katika makala iliyochapishwa na gazeti la Maariv kwamba Israel na baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu zinakabiliwa na kutengwa pakubwa kimataifa ambako hakujawahi kushuhudiwa.

Amesema, si tu Ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu bali aghalabu ya nchi duniani zimeungana dhidi ya Israel. 

Ben David amesema, nchi zaidi ya 140 zinajiandaa kuitambua rasmi nchi ya Palestina huku akitilia mkazo namna Israel inavyozidi kutengwa katika uga wa diplomasia.