Ehud Barak: Utawala wa Israel umo katika hatari ya kusambaratika kabisa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i132942-ehud_barak_utawala_wa_israel_umo_katika_hatari_ya_kusambaratika_kabisa
Waziri Mkuu wa zamani wa utawala haramu wa Israel Ehud Barak ameonya katika matamshi kuwa utawala wa Israel unaporomoka mbele ya macho ya Wazayuni.
(last modified 2025-11-08T10:48:35+00:00 )
Nov 08, 2025 10:28 UTC
  • Ehud Barak: Israel imo katika hali ya kusambaratika
    Ehud Barak: Israel imo katika hali ya kusambaratika

Waziri Mkuu wa zamani wa utawala haramu wa Israel Ehud Barak ameonya katika matamshi kuwa utawala wa Israel unaporomoka mbele ya macho ya Wazayuni.

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa, Barak amesema kuwa kuanguka huku hakuhusiani na mirengo ya kisiasa ya kulia au kushoto, Benjamin Netanyahu au wengine.

Alisema: "Tutashuhudia Israel ya kidemokrasia ya Kiyahudi-Kizayuni au udikteta wa ubaguzi wa rangi-dini, giza na fisadi ambao hatimaye utasababisha kuangamia Uzayuni na Israeli yenyewe."

Matamshi hayo ya Ehud Barak yanaashiria ukubwa migogoro ya ndani na kisiasa ndani ya utawala wa Kizayuni, jambo ambalo limewafanya hata shakhsia mashuhuri na wa zamani wa utawala huo kuwa na wasi wasi kuhusu mustakbali wake.

Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Israel hapo awali alitoa matamshi ya kukosoa vikali sera za serikali ya sasa, akisema kuwa uzembe wa serikali ya Netanyahu umeitia doa baya na kuichafua sura ya Israel, na kunahitajika kizazi kimoja ili kuisafisha.

Waziri mkuu wa zamani wa utawala wa Kizayuni wa Israel Ehud Barak amewahi kunukuliwa akisema pia kwamba, ana wasiwasi mkubwa kuwa yamkini utawala huo utaangamia kabla ya kuadhimisha mwaka wa 80 tokea uasisiwe.

Matamshi hayo ya Barak yanakuja wakati ambapo uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni unaonyesha kuwa vijana wengi raia wa Israel hawana matumaini kuhusu mustakabali wa utawala huo haramu.