Hamas yaanza rasmi shughuli zake nchini Algeria
Aug 29, 2016 23:03 UTC
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imetangaza kuanza rasmi shughuli zake huko Algeria.
Serikali ya Algeria imetangaza rasmi kukubali kuasisiwa na kufanya kazi ofisi ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas huko Algiers mji mkuu wa nchi hiyo. Ofisi hiyo ya Hamas iko tayari kuanza rasmi ghughuli zake huko Algeria.
Weledi wa mambo wa kieneo wameitaja hatua hiyo ya serikali ya Algeria ya kuafiki kufunguliwa ofisi ya Hamas kuwa itawakasirisha viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Aidha kushiriki Hamas katika uchaguzi wa mabaraza ya miji katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza kumeitia wasiwasi idara ya intelijinsia ya utawala wa Kizayuni.
Tags