Makundi ya Kizayuni yataka kuhitimishwa kukaliwa kwa mabavu Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i14848-makundi_ya_kizayuni_yataka_kuhitimishwa_kukaliwa_kwa_mabavu_palestina
Makundi kadhaa ya Wazayuni yametaka kukomeshwa kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 07, 2016 23:31 UTC
  • Makundi ya Kizayuni yataka kuhitimishwa kukaliwa kwa mabavu Palestina

Makundi kadhaa ya Wazayuni yametaka kukomeshwa kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina.

Makundi hayo ya Kizayuni ambayo yenyewe yanajiita kuwa yanaendesha harakati za amani yameashiria miaka kadhaa ya kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina na utawala wa Kizayuni na kutaka kufanyika kura ya maoni kuhusu kuhitimishwa suala hilo. Kampeni hiyo ya kutaka kuhitimisha kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina  ilianza juzi Jumanne huko Tel Aviv kwa ubunifu wa majenerali kadhaa wa zamani wa Kizayuni na harakati  inayojulikana kwa jina la Harakati ya Amani ya Ndani katika Ardhi Zinazokaliwa kwa mabavu. Makundi hayo ya Kizayuni yamesisitiza kufanyika kura ya maoni katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu ili kuhitimisha ukaliwaji mabavu huko Palestina na kurejeshwa amani kwa mujibu wa kuasisi serikali mbili. Wawakilishi wa kampeni hiyo wamemtumia barua Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel na kumtaka azingatie maoni ya wananchi.

Ramani ikionyesha nama Ardhi za Palestina zilivyoghusubiwa hatua kwa hatua na Israel