Wakimbizi wa Iraq warejea katika makazi yao
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i16600-wakimbizi_wa_iraq_warejea_katika_makazi_yao
Malefu ya familia za wakimbizi Wairaqi zimerejea katika makazi yao hapo awali baada amani na utulivu kurejea katika baadhi ya maeneo ya Iraq.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 03, 2016 10:48 UTC
  • Wakimbizi wa Iraq warejea katika makazi yao

Malefu ya familia za wakimbizi Wairaqi zimerejea katika makazi yao hapo awali baada amani na utulivu kurejea katika baadhi ya maeneo ya Iraq.

Wizara inayoshughulikia wakimbizi nchini Iraq imetangaza kuwa, Wairaqi elfu 64 na 325 wamerejea kwenye makazi yao baada ya kukombolewa miji ya mkoa wa al Anbar magharibi mwa Iraq kutoka mikononi mwa magaidi wa kundi la kitakfiri la Daesh.

Wimbi la kwanza la wakimbizi lilishuhudiwa huko Iraq mwaka 2006 baada ya kupamba moto mapigano ya baina ya makundi mbalimbali na uingiliaji wa nchi za nje katika masuala ya ndani ya nchi hiyo. Idadi ya wakimbizi wa Iraq mwaka huu wa 2016 imefikia zaidi ya milioni nne kufuatia uingiliaji kati  wa nchi za Magharibi na za Kiarabu katika masuala ya Iraq katika miaka ya hivi karibuni.

Mkoa wa al Anbar uliokombolewa kutoka mikononi mwa Daesh

Baadhi ya miji ya Iraq inapokea wimbi kubwa la wakimbizi kufuatia mashambulizi na mauaji yanayofanywa na kundi la kigaidi na kitakifiri la Daesh tangu mwezi Juni mwaka juzi hadi sasa. Kundi hilo linatenda jinai za kutisha dhidi ya raia wa Iraq kwa likiungwa mkono na baadhi ya nchi za Kiarabu na za Magharibi.

Wakati huo huo duru za usalama nchini Iraq zimeripoti kuwa, watu wanne wameuawa na wengine 11 kujeruhiwa katika mripuko wa bomu uliotokea leo kusini mwa Baghdad.