Marekani, Saudia, Israel ni waungaji mkono wa magaidi wa Daesh
Kamanda wa ngazi za juu wa jeshi nchini Syria amesema, kuna ushahidi wa kutosha kuwa Marekani, Saudi Arabia na Israel ni waungaji mkono wakuu wa magaidi wa ISIS (Daesh) huko Syria na Iraq.
Kwa mujibu wa televisheni ya Al Mayadeen, Kamanda wa Jeshi la Syria katika eneo la Aleppo amesema, wamepata taarifa za kijasusi zinazoonyesha wazi namna Marekani inayoshirikiana na Saudi Arabia na utawala wa Kizayuni wa Israel kuwahamisha magaidi wa ISIS kutoka mjini Mosul, Iraq na kuelekea nchini Syria.
Kamanda huyo wa Syria amesisitizia ulazima wa kuzifuchua nchi ambazo zinahusika katika kuwasaidia magaidi nchini humo.
Katika upande mwingine, Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imekaribisha oparesheni kubwa ya jeshi la Iraq mjini Mosul dhidi ya magaidi wa ISIS na kuongeza kuwa, Damascus inaunga mkono operesheni hiyo dhidi ya genge la kigaidi la Daesh.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imesema inaamini kuwa, vita dhidi ya ISIS na ugaidi ni vita dhidi ya wanaoyaunga mkono makundi hayo ya kigaidi.