Ubaguzi; moja ya nguzo kuu za utawala wa Kizayuni wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i18223-ubaguzi_moja_ya_nguzo_kuu_za_utawala_wa_kizayuni_wa_israel
Utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umejengeka juu ya siasa za kibaguzi na mauaji, mbali na kufanya ubaguzi dhidi ya Wapalestina umekuwa ukifanya vitendo kama hivyo dhidi ya raia wake jambo ambalo limeibua hasira na ghadhabu za Waisraeli.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 27, 2016 02:10 UTC
  • Ubaguzi; moja ya nguzo kuu za utawala wa Kizayuni wa Israel

Utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umejengeka juu ya siasa za kibaguzi na mauaji, mbali na kufanya ubaguzi dhidi ya Wapalestina umekuwa ukifanya vitendo kama hivyo dhidi ya raia wake jambo ambalo limeibua hasira na ghadhabu za Waisraeli.

Ripoti zinaonyesha kuwa, hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kufuatilia siasa zake za kibaguzi dhidi ya Wapalestina hususan hatua yake ya kuwafukuza kutoka katika ardhi zao, kujenga vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi, kujenga ukuta wa kibaguzi unaojulikana kama eti ukuta wa usalama na kuendeleza mzingiro dhidi ya Gaza licha ya kuyafanya maisha ya Wapalestina kuwa magumu pia inasukuma mbele gurudumu la malengo yake ya kibaguzi kwa kutekeleza vitendo vya ubaguzi dhidi ya raia wake.

Katika uwanja huo, Kituo cha Taarifa cha Bunge la Israel kilitangaza katika ripoti yake Jumanne ya juzi kwamba, matajiri katika jamii ya Israel wana nafasi mara nne zaidi ya kuingia Vyuo Vikuu au kupata vyeti vya juu ikilinganishwa na tabaka la watu masikini. Utafiti huo unaonyesha kuwa, asilimia 81 ya kazi zenye kipato kikubwa katika jamii ya Israel inapatiwa wanachuo wa familia tajiri huku kazi zenye kipato kidogo wakipewa wanachuo wanaotoka katika familia zenye uwezo mdogo wa kifedha.

Mafalanja wa Ethiopi wakiandamana huko Israel kupinga ubaguzi

Ripoti ya taasisi za Kizayuni na Wizara ya Kazi ya utawala huo ghasibu zinaonyesha kuwa, ubaguzi unashuhudiwa katika nguzo zote za utawala huo hususan katika idara za serikali na jeshi, jambo ambalo limewakasirisha mno Waisraeli. Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, kuendelea mwenendo huo kumeihatarisha mamlaka ya utawala huo. Ni kwa sababu hiyo ndio maana Mafalanja wa Ethiopia wanaoishi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina mara kadhaa wameandamana na kukusanyika mbele ya jengo la Bunge la Israel wakitaka kufutwa sheria za kibaguzi na kuweko haki sawa za kijamii.

Miongoni mwa hatua za kibaguzi za Isarel dhidi ya raia wa Kiyahudi ni kukataa kuandikishwa watoto wenye asili ya Afrika katika shule na vyuo vikuu vya utawala huo na kuwatengea njia maalumu za kupita wao tu. Katika jeshi la Israel pia, vyeo vya juu jeshini vimekuwa vikipatiwa wanajeshi wanaotoka katika familia mashuhuri na waliozaliwa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu au wenye asili ya Ulaya huku vyeo vya chini vikitengwa maalumu kwa ajili ya Mayahudi waliohajiri kutoka Afrika au wanaotoka katika familia masikini.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel

Hatua zote hizo za Israel ni mwendelezo wa hatua za kibaguzi nchini Afrika Kusini katika kipindi cha utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo wa Apartheid na vile vile miamala ya kibaguzi ya watu weupe dhidi ya weusi nchini Marekani.

Ukweli ni kuwa, Israel daima imekuwa ni jamii iliyojengeka juu ya matabaka ambapo Mayahudi wa Ashkenazi yaani wenye asili ya Magharibi wanahesabiwa kuwa jamii bora zaidi huku Mayahudi weusi ambao kikawaida wanatokea Ethiopia na ambao wanajulikana kama Mafalanja wamekuwa wakihesabiwa kuwa jamii ya daraja la chini kabisa, jambo ambalo lenyewe linaonyesha kwamba, Israel ni utawala wa ubaguzi wa rangi.

Bila shaka mambo hayo yanazidi kuweka wazi ukweli huu kwamba, jamii ya Kizayuni inaendeshwa kwa misingi ya ubaguzi mkubwa wa kijamii.