Jeshi la Israel lazongwa na tatizo la kutoroka askari jeshini
Makamanda wa jeshi la utawala ghasibu wa Israel wameeleza wasiwasi wao mkubwa kutokana na wimbi la kutoroka askari katika jeshi la nchi hiyo na mwenendo wa tabaka la vijana kuhepa suala la kutoa huduma jeshini.
Ofisi ya Uongozi wa Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel imezungumzia suala la kupungua idadi ya vijana wanaojiunga na jeshi la utawala huo na kueleza wasiwasi wale kuhusu ongezeko la idadi ya askari wanaotoroka jeshi, suala ambalo limekuwa mogoro mkubwa kwa Israel.
Ripoti zinasema nusu ya vijana wa Israel wamehepa kuingia jeshini kwa kutumia visingizio mbalimbali kama kujishughulisha na masuala ya kidini au sababu za kiafya.
Ripoti ya Ofisi ya Uongozi wa Jeshi la Israel inasema kuwa, asilimia 50 ya vijana wanahepa kujiunga na jeshi na sababau kuu zinaelezwa kuwa ni woga wa kuuliwa katika mapigano na wanaharakati wa Palestina au wapiganaji shupavu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon.
Utawala ghasibu wa Israel ambao kwa miaka mingi umekuwa ukiwalazimisha vijana kujiunga na jeshi na kuwatumia katika kudumisha ukatili na maiaji dhidi ya watu wa Palestina na nchi nyingine sasa unakabiliwa na mgogoro wa kutoroka askari na wanajeshi kutokana na baadhi ya wanajeshi hao kuelewa uhakika wa mambo.