Feb 28, 2016 02:27 UTC
  • Saudia yadondosha mabomu sokoni Yemen

Ndege za kivita za Saudi Arabia Jumamosi zilidondosha mabomu katika soko moja lenye idadi kubwa ya watu katika mkoa wa Sana'a nchini Yemen.

Walioshuhudia wanasema zaidi ya wato 60 waliuawa katika hujuma hiyo ya ndege za kivita za Saudia katika soko la wilaya ya Nehm, kaskazini mashriki mwa mji mkuu Sana'a.

Hujuma dhidi ya soko hilo ni katika mfululizo wa hujuma za Saudia dhidi ya maeneo ya raia nchini Yemen. Saudi Arabia ilianzisha mashambulizi ya kijeshi nchini Yemen tarehe 26 mwezi Machi mwaka jana, lengo likiwa ni kuisambaratisha harakati ya Ansarullah na kumrejesha madarakani Rais mtoro na aliyejiuzulu wa Yemen, Abdu-Rabuh Mansour Hadi.

Takwimu zainaonesha kuwa katika hujuma za kinyama za Saudia dhidi ya Yemen, watu karibu 8,400 wameuawa wengi wao wakiwa ni raia hasa watoto na wanawake.

Idadi ya watoto Wayemeni waliouawa katika hujuma za Saudia ni 2,236. Aidha Saudia inadondosha mabomu katika mahospitali, misikiti, shule, viwanda, madaraja na miundombinu yote ya Yemen. Saudia pia inatumia mabomu yaliyopigwa marufuku katika hujuma zake za kuogofya dhidi ya wananchi wa Yemen.

Tags