Kuzidi kuwa mkubwa mgogoro wa kiuchumi wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i21394-kuzidi_kuwa_mkubwa_mgogoro_wa_kiuchumi_wa_israel
Taasisi ya utawala wa Kizayuni ya Latite imefichua kuwa, karibu watu milioni 2.5 wakazi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wanaishi chini ya mstari wa umaskini.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Dec 14, 2016 04:00 UTC
  • Kuzidi kuwa mkubwa mgogoro wa kiuchumi wa Israel

Taasisi ya utawala wa Kizayuni ya Latite imefichua kuwa, karibu watu milioni 2.5 wakazi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wanaishi chini ya mstari wa umaskini.

Kigezo kilichotumiwa na taasisi hiyo ya Kizayuni kupiga kiwango hicho cha ukata na umaskini ni kuangalia uwezo wa watu wa kudhamini mahitaji yao ya dharura katika maisha kama vile makazi, elimu na usalama wa chakula pamoja na ughali wa bidhaa. Takwimu hizo za kufedhehesha, zinatofautiana kikamilifu na ripoti rasmi za utawala wa Kizayuni zilizotolewa na Shirika la Bima ya Taifa ya utawala huo zinazodai kuwa kiwango cha ukata na umaskini ndani ya utawala wa Kizayuni wa Israel ni watu milioni 1.7.

Maandamano ya kupinga siasa mbovu za Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, mjini Tel Aviv

Ni jambo lililo wazi kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unachuja sana habari na kukwepa kutoa takwimu sahihi za kiwango cha ukata na ufukara ndani ya utawala huo unaozikalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina kutokana na kuhofia kuongezeka wimbi la Wazayuni wanaozikimbia ardhi hizo za Palestina na vile vile kuficha utawala wa Kizayuni aibu ya kushindwa kuwatatulia migogoro ya kiuchumi Wazayuni hao. Kwa mujibu wa taasisi ya Latite, kati ya Wazayuni milioni nane wanaoishi kwenye ardhi za Palestina zilizotekwa mwaka 1948, kuna watoto milioni moja wanaoishi kwenye ukata wa kufurutu mipaka. Kabla ya hapo jarida la masuala ya uchumi la GLOBS linalochapishwa mjini Tel Aviv liliripoti kuwa, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kiwango cha mashirika ya kiuchumi ya Israel yaliyotangaza kufilisika kimeongezeka kwa asilimia 55.

Umaskini na ukata wa kupindukia katika jamii ya Israel umeongezeka sana hususan katika miongo ya hivi karibuni na mara nyingi Wazayuni wamekuwa wakifanya maandamano ya mamia ya maelfu ya watu kulalamikia hali mbaya ya kiuchumi. Licha ya utawala wa Kizayuni kuwa na bajeti kubwa ya kifedha kutokana na uungaji mkono wa kila namna wa madola ya Magharibi na kutokana na wizi na uporaji wa kupindukiwa unaofanywa na dola hilo pandikizi katika ardhi za Wapalestina, lakini pamoja na hayo yote unashindwa kujitoa kwenye kitanzi ya migogoro isiyoisha ya kiuchumi kutokana na sehemu kubwa ya bajeti yake kutengwa kwa ajili ya kujipanua na masuala ya kijeshi. Licha ya Wazayuni kuishi kwenye hali ngumu sana ya kiuchumi, lakini utawala wa Kizayuni hauko tayari kupunguza gharama zake za kijeshi na wala kuachana na siasa zake za kujipanua na jambo hilo kwa hakika linazidi kuonesha sura halisi ya ushari na dhulma ya utawala ghasibu wa Kizayuni.

Fauka ya hayo, matukio ya ndani ya utawala wa Kizayuni yanabainisha kuwa, migogoro ya ndani ya utawala huo pandikizi ikiwemo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii imeongezeka sana katika miezi ya hivi karibuni na hilo linazidi kuthibitisha namna Wazayuni wakazi wasivyoridhishwa na siasa za Israel. Mizozo ya kijamii na kuzidi kupanuka ukata na umaskini pamoja na kushtadi wimbi la malalamiko ndani ya utawala wa Kizayuni hivi sasa kumepiga kengele ya hatari ndani ya utawala huo. Mgogoro ni mkubwa kiasi kwamba taasisi mbalimbali za kiuchumi za Israel zimeshindwa kuficha jambo hilo.

Mauti kwa utawala wa Kizayuni wa Israel

 

Takwimu zilizotolewa na duru mbalimbali zinaonesha kuwa, Israel hivi sasa inapitia kipindi kigumu mno cha migogoro ya kisiasa na kiuchumi tangu kuasisiwa kwake. Mashirika tofauti za kiuchumi za utawala wa Kizayuni zimeingia kwenye mstari wa kufilisika katika miezi ya hivi karibuni na hivyo kulazimika kuwafukuza kazi idadi kubwa ya wafanyakazi wake. Hali hiyo inazidi kuwafedhehesha viongozi wa utawala wa Kizayuni ambao waliwashawishi Mayahudi kuhamia kwenye ardhi walizoporwa Wapalestina kwa tamaa ya kuishi kwenye ardhi za mito ya maziwa na asali. Hali ni mbaya kiasi kwamba wimbi la Wazayuni wanaozikimbia ardhi za Palestina na kurejea walikotoka linaongezeka siku baada ya siku na hilo linazidi kuharakisha kusambaratika kikamilifu utawala huo pandikizi.