Rhodes: White House imefeli katika kuhuisha mazungumzo ya Israel-Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i22117-rhodes_white_house_imefeli_katika_kuhuisha_mazungumzo_ya_israel_palestina
Naibu Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani amesema kuwa, siasa za White House zimefeli na kushindwa katika suala la mazungumzo ya mapatano kati ya Israel na Wapalestina.
(last modified 2026-08-17T09:53:57+00:00 )
Dec 25, 2016 12:19 UTC
  • Rhodes: White House imefeli katika kuhuisha mazungumzo ya Israel-Palestina

Naibu Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani amesema kuwa, siasa za White House zimefeli na kushindwa katika suala la mazungumzo ya mapatano kati ya Israel na Wapalestina.

Ben Rhodes amesema kuwa juhudi zote zilizofanywa na Rais Barack Obama wa Marekani kwa ajili ya kuhusisha mazungumzo ya mapatano kati ya Israel na Wapalestina zimeshindwa kutokana na vizingiti na mikingamo inayowekwa siku zote na viongozi wa Isarel. 

Benjamin Netanyahu

Matamshi hayo ya Naibu Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani yametolewa baada ya maafisa wa utawala haramu wa Israel hususan Waziri Mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu kumshambulia Rais anayemaliza muda wake wa Marekani kuwa ameisaliti Israel kwa sababu ya kutotumia kura ya veto kuzuia azimio nambari 2334 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo limeiamuru Isarel kusitisha mara moja ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. 

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Ijumaa iliyopita na katika hatua isiyo ya kawaida, Baraza la Usalama la UN limepasisha azimio hilo linalolaani ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi zilizoghusubiwa za Palestina na kutaka ukomeshwe. Azimio hilo limepashwa na nchi 14 wanachama wa Baraza la Usalama mkabala wa kura moja tu ya Marekani ambayo imekataa kulipigia kura.