Hizbullah: Iran ndio iliyohuisha upya kadhia ya Palestina duniani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i25318-hizbullah_iran_ndio_iliyohuisha_upya_kadhia_ya_palestina_duniani
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon amesema kuwa, hii leo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kutumia nyenzo za uwezo, uthabiti na bila ya kuwa na utegemezi, imeweza kuibadilisha sura ya eneo la Mashariki ya Kati, kufungua milango ya ushindi sambamba kuhuisha upya kadhia ya Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 18, 2017 12:49 UTC
  • Hizbullah: Iran ndio iliyohuisha upya kadhia ya Palestina duniani

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon amesema kuwa, hii leo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kutumia nyenzo za uwezo, uthabiti na bila ya kuwa na utegemezi, imeweza kuibadilisha sura ya eneo la Mashariki ya Kati, kufungua milango ya ushindi sambamba kuhuisha upya kadhia ya Palestina.

Sheikh Naim Qassim, ameyasema hayo katika hafla iliyopewa jina la 'Mustakbali wa Umma katika Anga ya Mabadiliko baada ya Mapinduzi' ambayo imeandaliwa na kitengo cha utamaduni cha Iran mjini Beirut, Lebanon. 

Bendera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Harakati ya Hizbullah

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah amesema kuwa, kupitia uungaji mkono wa Iran kwa harakati hiyo, Waarabu na Waislamu wanaweza kutumia bendera hiyo kuliongoza eneo la Mashariki ya Kati kuelekea kwenye kheri na saada. Sheikh Naim Qassim amefafanua kuwa, Harakati ya Hizbullah inajifakharisha sana kuwa na mahusiano ya karibu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa kuwa inashuhudia kutoka nchi hii kheri, muqawama, utukufu na ushindi.

Bendera ya Harakati ya Hizbullah

Sambamba na kusisitiza juu ya ulazima wa kushirikiana na Iran kwa ajili ya kulisambaratisha dondandugu la saratani la Uzayuni amesema kuwa, bila kuwa na tamaa ya kitu, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imenyoosha mkono wa msaada kwa ajili ya kuyaokoa mataifa na nchi za dunia na kuyatakia kheri na saada mataifa hayo.

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah amesema kuwa Hizbullah iliweza kujipatia ushindi wake wa kwanza mwaka 2000 katika kukabiliana na adui wa Kizayuni kwa kuikomboa ardhi ya Lebanon na mwaka 2006 pia ikalipigisha magoti jeshi la utawala huo haramu wa Israel.../