Mbinu mpya za Israel za kuwaua viongozi wa Hizbullah na Hamas
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i25682-mbinu_mpya_za_israel_za_kuwaua_viongozi_wa_hizbullah_na_hamas
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa utawala wa Kizayuni amewatishia viongozi wa Hizbullah ya Lebanon na wale wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS kuwa Israel itatumia mbinu mpya za kuwaua.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Feb 26, 2017 23:17 UTC
  • Mbinu mpya za Israel za kuwaua viongozi wa Hizbullah na Hamas

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa utawala wa Kizayuni amewatishia viongozi wa Hizbullah ya Lebanon na wale wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS kuwa Israel itatumia mbinu mpya za kuwaua.

Mtandao wa habari wa Felestin al Yaum umemnukuu Ayoob Kara, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Kieneo wa Israel akisema jana Jumapili kwamba, hivi sasa utawala wa Israel unatengeneza roboti ambaye atatumika kwa ajili ya kuwaua viongozi wa Hizbullah ya Lebanon na viongozi wa makundi ya muqawama ya Palestina.

Kiongozi huyo wa Israel ameashiria namna utawala wa Kizayuni ulivyofeli katika vita na wanamapambano wa Palestina huko Ghaza na kusema, hatupaswi kuruhusu kujikariri katika vita vipya, yale yaliyowakumba wanajeshi wa Israel kwenye vita vilivyopita.

Hivi karibuni pia, gazeti la Kizayuni la Maariv lilitoa ripoti kuhusiana na siasa za mauaji ya kigaidi za utawala wa Kizayuni dhidi ya viongozi wa Palestina na Hizbullah na kusema kuwa, siasa hizo zimefeli.

Gazeti la Kizayuni la Maáriv

 

Gazeti hilo la Kizayuni limesema, hatuwezi kujivunia siasa hizo na wala hazina uwezo wa kuzuia opereseheni za Wapalestina dhidi ya Israel.

Kwa upande wake, Avigdor Lieberman, waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni amelitaka baraza la mawaziri la Israel kutekeleza siasa za kuwaua viongozi wa muqawama wa Palestina kwenye Ukanda wa Ghaza.

Katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, utawala wa Kizayuni umeua kigaidi viongozi wasiopungua 16 wa Kipalestina na Kiarabu katika maeneo tofauti duniani.