Wapalestina waliunga mkono jeshi na serikali ya Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i26548-wapalestina_waliunga_mkono_jeshi_na_serikali_ya_syria
Mwakilishi wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina hapa mjini Tehran amesema kuwa, makundi ya muqawama ya Palestina yanaliunga mkono jeshi na serikali ya Syria katika kukabiliana na uchokozi wa utawala wa Kizayuni na pia kukomboa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Mar 18, 2017 12:20 UTC
  • Nasser Abu Sharif, Mwakilishi wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina mjini Tehran, Iran
    Nasser Abu Sharif, Mwakilishi wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina mjini Tehran, Iran

Mwakilishi wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina hapa mjini Tehran amesema kuwa, makundi ya muqawama ya Palestina yanaliunga mkono jeshi na serikali ya Syria katika kukabiliana na uchokozi wa utawala wa Kizayuni na pia kukomboa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel.

Nasser Abu Sharif amesema hayo katika mahojitano aliyofanyiwa na shirika la habari la Qudsuna na huku akigusia mashambulizi ya jana asubuhi ya ndege za utawala wa Kizayuni nchini Syria na kutunguliwa ndege moja ya Israel amesema kuwa, uvamizi huo unazidi kuthibitisha jinsi utawala wa Kizayuni ulivyo khabithi.

Mwakilishi wa harakati ya Jihadul Islami wa Palestina nchini Iran ameongeza kuwa, uwezo wa jeshi la Syria wa kugundua, kufuatilia na kushambulia ndege za Israel na kutungua ndege moja tena katika wakati mfupi, unaonesha uimara wa jeshi la Syria ambalo limefanikiwa kufanya hivyo licha ya kwamba liko vitani kwa miaka kadhaa mfululizo likipambana na makundi yanayofanya uharibifu mkubwa nchini Syria.

Nembo ya jeshi la Syria

 

Amesema, uwezo wa jeshi la Syria wa kujibu haraka sana mashambulizi ya anga ya jana Ijumaa ya Israel unaonesha kuweko mabadiliko makubwa katika uwezo wa kujihami wa jeshi la Syria na tunaweza kusema kuwa, nchi hiyo hivi sasa imerejea katika hali yake ya kawaida. Amesema, kuanzia sasa kambi ya muqawama itaendelea kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa nguvu kubwa zaidi.

Kiongozi huyo mwandamizi wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina aidha amezitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu kuwa pamoja na wananchi wa Syria na kuelekeza nguvu zao katika kukabiliana na pande ambazo lengo lake ni kuvunja nguvu za kijeshi za nchi za Kiarabu na Kiislamu na kuzibakisha kwenye kinamasi cha vitendo vya kigaidi.