Wananchi wa Bahrain waandamana kumuunga mkono Sheikh Issa Qassim
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i27434-wananchi_wa_bahrain_waandamana_kumuunga_mkono_sheikh_issa_qassim
Wananchi wa maeneo mbalimbali ya Bahrain wamefanya maandamano jana kumuunga mkono na kuonyesha mshikamano wao kwa Sheikh Issa Qassim mwanazuoni mashuhuri wa ngazi ya juu wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 07, 2017 23:14 UTC
  • Wananchi wa Bahrain waandamana kumuunga mkono Sheikh Issa Qassim

Wananchi wa maeneo mbalimbali ya Bahrain wamefanya maandamano jana kumuunga mkono na kuonyesha mshikamano wao kwa Sheikh Issa Qassim mwanazuoni mashuhuri wa ngazi ya juu wa nchi hiyo.

Wananchi wa Bahrain katika miji mbalimbali ya nchi hiyo ukiwemo mji wa al Diraz na katika vitongoji vya al Nuwaidrat, al Jifram, al Maamir, Sitrah, Sarah, na vinginevyo jana Ijumaa waliandamana kumunga mkono Sheikh Issa Qassim kufuatia kuendelea upinzani na malalamiko ya wananchi dhidi ya vitendo vya utawala wa Aal Khalifa. Wafanya maandamano hao kwa mara nyingine tena walitangaza uungaji mkono wao kwa wahanga wote wa mauaji yanayofanywa na utawala wa Aal Khalifa huko Bahrain.

Sheikh Issa Qassim 

Utawala wa Bahrain mwezi Juni mwaka jana ulimfutia uraia Sheikh Issa Qassim mwanazuoni mashuhuri wa nchi hiyo; kitendo kilichokabiliwa na radiamali kali ndani ya Bahrain kwenyewe na kutoka maeneo mbalimbali ya dunia. Vijana katika mji wa Sitra pia waliandamana jana Ijumaa kulalamikia hukumu ya kunyongwa iliyotolewa kwa vijana wawili; maandamano ambayo yalikabiliwa na ukandamizaji na kushambuliwa na askari eti wa usalama wa Bahrain ambao walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji. 

Vijana katika kitongoji cha al Sitra Bahrain wakipambana na polisi