Amnesty International yaanzisha kampeni ya kumuungamkono kiongozi wa upinzani Bahrain
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i27756-amnesty_international_yaanzisha_kampeni_ya_kumuungamkono_kiongozi_wa_upinzani_bahrain
Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limeanzisha kampeni ya umma inayoutaka utawala wa Bahrain kumuachia huru haraka na bila ya masharti Sheikh Ali Salman, mwanazuoni mashuhuri wa nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 14, 2017 03:46 UTC
  • Amnesty International yaanzisha kampeni ya kumuungamkono kiongozi wa upinzani Bahrain

Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limeanzisha kampeni ya umma inayoutaka utawala wa Bahrain kumuachia huru haraka na bila ya masharti Sheikh Ali Salman, mwanazuoni mashuhuri wa nchini humo.

Taarifa kuhusu kampeni hiyo ambayo ilitumwa jana kwenye tovuti ya Amnesty International imeeleza kuwa, utawala wa Manama unapasa kushinikizwa ili umuondoe hatiani Sheikh Salman ambaye ni mfungwa wa dhamiri. 

Wananchi wakiandamana kumuunga mkono Sheikh Salman 

Taarifa ya shirika hilo  imeongeza kuwa, mwanazuoni huyo wa Kishia ambaye ni mkuu wa Jumuiya ya Kitaifa ya Kiislamu ya al Wifaq iliyopigwa marufuku na serikali ya Bahrain amefungwa jela kwa kudai haki yake ya kujieleza kwa njia ya amani. Kiongozi huyo wa upinzani amefungwa jela tangu mwaka 2014 kutokana na kile kilichotajwa na watawala wa Manama kuwa kwa kosa la kuwakashifu maafisa wa serikali na kuchochea machafuko kupitia hotuba zake zilizoulenga utawala ulioko madarakani.