Assad: Nchi za Magharibi zinazuia uchunguzi kuhusu
(last modified Fri, 21 Apr 2017 07:03:19 GMT )
Apr 21, 2017 07:03 UTC
  • Assad: Nchi za Magharibi zinazuia uchunguzi kuhusu

Rais Bashar la al-Assad wa Syria anasema nchi za Magharibi zinalenga kuzuia uchunguzi huru kuhusu kile kilichotajwa kuwa ni hujuma ya silaha za kemikali nchini humo hivi karibuni.

Katika mahojiano na Shirika la Habari la Sputnik la Russia, Assad amesema nchi za Magharibi zina hofu kuwa, uchunguzi utabaini tukio hilo la kemikali lilikuwa ni njama kwa ajili ya malengo maalumu. Ameongeza kuwa, Syria imeshauandikia barua Umoja wa Mataifa  ikitaka ujumbe wa umoja huo utumwe kuchunguza kilichojiri Khan Shaykhun. Amesema Umoja wa Mataifa haujatuma ujumbe kwa sababu nchi za Magharibi na hasa Marekani imezuia ujumbe huo kufika Syria kwani ukweli utabainika kuhusu kauli zao potofu kuhusu yaliyojiri Khan Shaykhun. Amesema kuwa ukweli huo utabaini kuwa Marekani ilifanya makosa kuvurumisha makombora ya Tomahawk dhidi ya uwanja wa ndege wa kijeshi wa Shayrat.

Uwanja wa ndege wa Shayrat uliolengwa na Marekani

Itakumbukwa kuwa mnamo Aprili 7, Marekani ilivurumisha makombora 59  kutoka katika meli zake mbili za kivita zilizoko katika bahari ya Mediterania na kukishambulia kituo cha jeshi la anga la Syria katika eneo la Shayrat katika mkoa wa Homs na kuua watu tisa wakiwemo watoto wanne na kujeruhi wengine kadhaa. 

Rais Donald Trump wa Marekani alitoa amri ya kufanywa shambulizi hilo, kwa madai ya uongo ya kuwa serikali ya Syria ilitumia silaha za kimekilai huko Khan Shaykuhu na kuua watu zaidi ya 80 manmo Aprili 4. Serikali ya Syria imekanusha vikali madai hayo na mara kadhaa imetaka uchunguzi wa kimataifa ufanyike kuhusu jambo hilo.

Rais Assad ameema picha za tukio la Khan Shaykhun zilikuwa bandia na kuongezwa kuwa nchi za Magharibi zilichukua maamuzi kwa mujibu wa taswira zilizosambazwa na kundi la kigaidi la Al Qaeda.