Usalama mdogo Marekani, raia wavunja rekodi za kununua silaha za kujilinda
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i28598-usalama_mdogo_marekani_raia_wavunja_rekodi_za_kununua_silaha_za_kujilinda
Ikiwa ni katika kuthibitisha kuwa hali ya usalama nchini Marekani imezidi kuwa mbaya hasa baada ya kuingia madarakani Rais Donald Trump, biashara ya silaha za moto nchini humo imeongezeka sana kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa mfano wake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 03, 2017 10:15 UTC
  • Usalama mdogo Marekani, raia wavunja rekodi za kununua silaha za kujilinda

Ikiwa ni katika kuthibitisha kuwa hali ya usalama nchini Marekani imezidi kuwa mbaya hasa baada ya kuingia madarakani Rais Donald Trump, biashara ya silaha za moto nchini humo imeongezeka sana kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa mfano wake.

Mtandao wa Inteneti wa Washington Free Beacon umeripoti habari hiyo na kunukuu ripoti ya uchunguzi wa polisi ya FBI ya Marekani ikisema kuwa, kiwango cha uuzaji wa silaha za moto katika mwezi ulioisha wa Aprili kimepindukia kiwango cha biashara hiyo katika mwezi kama huo mwaka jana.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika mwezi wa Aprili 2017 pekee, kumeuzwa silaha za moto zaidi ya milioni mbili na 45 elfu, kiwango ambacho kimevunja rekodi ya mauzaji ya silaha nchini humo. Kiwango hicho kinaoensha kuweko ongezeka la silaha laki moja ikilinganishwa na mwezi Aprili 2016. Manunuzi hayo ya silaha aidha yanaonesha kuweko ongezeka la silaha laki nne ikilinganishwa na manunuzi kama hayo mwezi Machi 2016.

Rais Donald Trump wa Marekani

Ripoti ya uchunguzi wa polisi wa FBI inaonesha kuwa, uuzaji wa silaha umeongezeka nchini humo tofauti na inavyotangazwa na vyombo vya habari ambayo katika katika miezi ya hivi karibuni vimekuwa vikidai kuwa biashara hiyo inaendelea kupungua.

Matukio ya kuuana kwa kupigana risasi ni ya kila siku nchini Marekani. Maelfu ya watu wanauawa na kujeruhiwa katika matukio hayo kila mwaka.