May 09, 2017 13:39 UTC
  • Magaidi wakufurishaji wauana katika viunga vya Damascus

Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa katika safu ya makundi ya kigaidi na ukufurishaji kufuatia kushadidi tofauti baina ya genge la Jaishul-Islam na Jab'hatu Nusra eneo la Ghouta al-Sharqiya la mji mkuu wa nchi hiyo Damascus.

Kabla ya hapo tahere 28 April mwaka huu, mapigano makali yalishuhudiwa baina ya kundi la kigaidi la Jab'hatu Nusra na Failaqu al-Rahman na kundi la Jaishul-Islami, ambapo kwa akali magaidi 100 waliuawa. Inaelezwa kuwa, sababu ya kuibuka tena mapigano makali baina ya makundi hayo ya kigaidi yanayopata uungaji mkono kutoka Marekani, Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu ikiwemo Saudia na Imarati, ni hatua ya genge la Jab'hatu Nusra ya kushambulia wapiganaji wa kundi la Jaishul-Islam.

Magaidi wa Kiwahabi wakishambuliana

Aidha mapigano yaliyojiri wiki iliyopita baina ya makundi tajwa, yalipelekea makumi ya wapiganaji wa pande mbili kuuawa na wengine kujeruhiwa. Inafaa kuashiria kuwa kushindwa mtawalia kwa makundi ya kigaidi nchini Syria katika pande tofauti na kadhalika kusonga mbele kwa jeshi na harakati ya muqawama dhidi ya magaidi, kumeibua tofauti kubwa baina ya viongozi wa makundi ya kigaidi na hivyo kuanza kushambuliana.

Kiongozi wa genge la Jayshul Islam, Zahran Alloush aliyeuawa mwaka 2015

Kundi la Jayshul Islam ni miongoni mwa magenge makubwa ya kigaidi nchini Syria, huku likiwa linapata uungaji mkono wa moja kwa moja kutoka Saudi Arabia. Kiongozi wa genge hilo Zahran Alloush aliangamizwa kwenye shambulio la ndege za Syria mwezi Disemba 2015. Saudi Arabia ilitangaza hadharani kukasirishwa mno kwa kuuliwa gaidi huyo.

Tags