Mashambulizi ya Saudia nchini Yemen, yasababisha kuenea maradhi baina ya watoto
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i29010-mashambulizi_ya_saudia_nchini_yemen_yasababisha_kuenea_maradhi_baina_ya_watoto
Kuendelea vita na mzingiro wa kila upande unaofanywa na Saudi Arabia kupitia ndege za kivita za nchi hiyo huko Yemen, kumesababisha kuenea maradhi baina ya watoto wa taifa hilo masikini la Kiarabu, kiasi kwamba kila dakika 10 mtoto mmoja hufariki dunia kutokana na maradhi hayo.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
May 12, 2017 22:04 UTC
  • Mashambulizi ya Saudia nchini Yemen, yasababisha kuenea maradhi baina ya watoto

Kuendelea vita na mzingiro wa kila upande unaofanywa na Saudi Arabia kupitia ndege za kivita za nchi hiyo huko Yemen, kumesababisha kuenea maradhi baina ya watoto wa taifa hilo masikini la Kiarabu, kiasi kwamba kila dakika 10 mtoto mmoja hufariki dunia kutokana na maradhi hayo.

Mtandao wa habari wa Al-Ahd wa nchini Lebanon umefichua kuwa, kuendelea mashambulizi ya anga ya Saudia katika miundombinu, mahospitali, shule na makazi ya raia na kadhalika mzingiro wa kila upande wa nchi hiyo vamizi dhidi ya Yemen, kumepelekea kuenea maradhi kama vile kipindupindu na magonjwa mengine yanayoteketeza maisha ya watoto.

Watoto wa Yemen wanaokabiliwa na maafa ya halaiki

Kadhalika mtandao huo wa habari wa al-Ahd umeandika kuwa, mashambulizi hayo ya Saudia yamesababisha huduma za afya na matibabu nchini Yemen kukumbwa na mgogoro mkubwa. Hayo yanajiri katika hali ambayo, hivi karibuni Shirika la Afya Duniani WHO lilitangaza kuibuka ugonjwa wa kipindupindu na maradhi mengine baada ya mashambulizi ya Saudia nchini Yemen ambapo hadi sasa kwa akali watu 34 wamepoteza maisha kwa maradhi hayo. Mara nyingi ugonjwa wa kipindupindu huambukizwa kupitia uchafu wa maji ya kunywa ambapo inapotokea mgonjwa kuchelewa kupata huduma ya matibabu haraka, hupoteza maisha kwa kipindi cha saa chache.

Maji machafu yanayosababisha maradhi kwa raia wa Yemen

Siku chache zilizopita, Muhammad al-As'adi Msemaji wa Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF alinukuliwa akisema kuwa, katika kipindi cha siku 12 zilizopita, kuliripotiwa kesi 82 za maambukizi ya virusi vya maradhi ya kipindupindu nchini Yemen ambapo nusu ya waathirika wa maradhi hayo walikuwa ni watoto wadogo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ugonjwa huo umeikumba mikoa 13 ya Yemen hadi sasa.

Miongoni mwa jinai ndogo za Saudia nchini Yemen