Syria yakanusha madai bandia ya Marekani dhidi yake
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i29172-syria_yakanusha_madai_bandia_ya_marekani_dhidi_yake
Syria imekanusha vikali madai bandia yaliyotolewa na Marekani kwamba serikali ya Damascus imejenga gereza la kuwachoma moto wafungwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 16, 2017 09:47 UTC
  • Syria yakanusha madai bandia ya Marekani dhidi yake

Syria imekanusha vikali madai bandia yaliyotolewa na Marekani kwamba serikali ya Damascus imejenga gereza la kuwachoma moto wafungwa.

Shirika rasmi la habari la SANA limenukuu taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria ikisema kuwa, madai hayo yasiyo na msingi ya Marekani ni mwendelezo wa taifa hilo la kibeberu wa kubuni hadithi za urongo kama za "Hollywood".

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, ni kawaida kwa Marekani kuzusha propaganda na kueneza habari za urongo wanapotaka kuhalalisha maovu yao na kwamba madai hayo yanapania kuhahalisha uvamizi wake dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Marekani ilivyofyatua makombora ya Tomahawk dhidi ya Syria

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imebainisha kuwa, Washington inataka kutumia madai hayo bandia ili izidi kupata sababu za kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.

Radiamali hii ya Syria imetolewa siku moja baada ya Marekani kueneza habari za propaganda kuwa gereza la kijeshi la Saydnaya lililoko yapata kilomita 30 kaskazini mwa mji mkuu Damascus linatumiwa na serikali ya Rais Bashar al-Assad kuwateketeza moto maelfu ya wafungwa na raia wa kawaida waliouawa na vyombo vya dola, ili kuficha mauaji hayo.

Itakumbukwa kuwa, hivi karibuni Marekani ilivurumisha makombora 59 kutokea meli zake mbili za kivita katika bahari ya Mediterania na kukishambulia kituo cha jeshi la anga la Syria katika eneo la Shayrat katika mkoa wa Homs na kuua watu tisa wakiwemo watoto wanne na kujeruhi wengine kadhaa, kwa kisingizio bandia kuwa serikali ya Syria iliua watu zaidi ya 80 kwa hujuma ya silaha za kemikali dhidi ya raia wa nchi hiyo, suala ambalo lilikanushwa vikali na Damascus.