Wazayuni wamuua shahidi Mpalestina mwingine
Mpalestina mwingine amekufa shahidi siku chache baada ya kufyatuliwa risasi na wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kujeruhiwa vibaya.
Muhand Abdulrahman Abu Safaqa, raia Mpalestina mwenye umri wa miaka 45 mkaazi wa Tulkaram amekufa shahidi Alkhamisi usiku ambapo alipiigwa risasi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel siku ya Jumanne.
Kwingineko Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas amesema amekutana na mjumbe maalumu wa Marekani Jason Greenblatt mjini Ramallah. Mmarekani huyo ni mpatanishi baina ya wafungwa wa Palestina na Israel. Inasemekana kuwa analenga kuhakikisha utalawa wa Kizayuni unaheshimu haki za wafungwa na mateka wa Kipalestina ambao wanasusia kula chakula kwa muda wa karibu siku 40 sasa.
Wakati huo huo Alison Weir mwandishi wa habari mashuhuri wa Marekani ambaye anaongoza kampeni dhidi ya Uzayuni amesema kuwa, kutokana na lobi ya Israel na Marekani na kuhodhi kwake madaraka, habari kuhusu Palestina zinabanwa sana katika vyombo vya habari vya Marekani. Amesema habari zote za Palestina nchini Marekani zinaandikwa kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.